VIDEO YA MWANAMUZIKI AY - PARTY ZONE KUTOKA THIS WEEK !!!


Rapper mwenye mafanikio makubwa nchini Tanzania, Ambwene Yesaya amesema video yake mpya inatoka wiki hii.
Video hiyo ambayo ilifanyika mwishoni mwa mwezi uliopita mjini Johannesburg Afrika Kusini imefanywa na kampuni ya God Father Productions inayomilikiwa na mnaijeria Mike Ogeke.
Kupitia Twitter jana AY amesema, “This week m goin to release my nu video “Party Zone” feat @Marcochali ..Film Standard broda,filmed by @I_Am_Godfather RT @ChrisIncc: @AyTanzania Yessır! Eyes on the prıze…”
Video ya wimbo huo uitwao ‘Party Zone’ uliotengenezwa na Marco Chali wa MJ Records itaingia kwenye orodha ya video zenye gharama zaidi kuwahi kufanywa na msanii wa Tanzania.
Kiasi cha dola 20,000 kimemtoka AY ambacho ni zaidi ya shilingi milioni 30 za Tanzania huku gharama hiyo ikiwa ya video peke yake.
Ukijumlisha nauli ya AY na Marco Chali ya kwenda Afrika Kusini na kurudi, malazi na mambo mengine gharama inakuwa kubwa zaidi.
Kampuni hiyo inasifika kwa video ilizowahi kuwafanyia P-Square, Flavor na wasanii wengine wakubwa wa Nigeria na Afrika Kusini.....BIG UP TO AY