DJ FETTY AIWAKIRISHA TANZANIA VYEMA KWENYE BIG BROTHER AFRICA..NA KUKUBALIKAJUZI Dj Fetty wa Tanzania ameithibitishia Afrika kuwa muziki anaujua, baada ya kuangusha ngoma za ukweli kwenye live show ya Big Brother.
Akiwa Dj wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kuwahi kupata heshima hiyo ya kuburudisha mamilioni ya watazamaji wa ukumbuni kwenye nyumba ya Big Brother pamoja na wale wanaoangalia kupitia TV, Fetty aliyekuwa anajiamini vya kutosha amepokea pongezi kutoka kwa wapenzi wa BBA barani kote.
Katika ukurasa rasmi wa Big Brother Afrika jana kumewekwa status iliyosema, “Our first lady DJ on the Big Brother stage…and she is trailblazing!” na kufuatiwa na comments nyingi za kumsifia kwa kazi nzuri:
Hongera sana Dada yetu kwa kutuwakirisha vyema..Ingawa mwakirishi wetu alitolewa wa kwanza kwenye BBA...I am a big fan of yours by the way Miss DJ!
.