MWANAMUZI WA KIZAZI KIPYA " AMINI " AKIPAGAWISHA FIESTA TABORA.....JAMAA BALAA!

WANAMUZIKI KUTOKA KENYA "P-UNIT" WALIWASHA MOTO WASHINGTON DMV WAKISINDIKIZWA NA MTANZANIA "AJ UBAO"


P-Unit walizikonga nyoyo za washabiki wliojitokeza kwa wingi katika club ya Kama iliyopo Beltsvile Maryland.Wanamuziki hao waliweza kuwaimbisha washabiki note kwa note Vibao vyao Vikali kama Gentleman,You Guy na Kare pamoja na Nyimbo zao nyingi mpya.Wanamuziki hawa Waliletwa DMV na Timu ya Mapromota kutoka Kenya Wakishirikiana na Kampuni ya Promosheni ya Watanzania ya DMKGLOBALPROMOTIONS.COM .
Baada ya Kumaliza Show hiyo ya DC walipanda ndege kuelekea Los Angeles California ambapo watafanya show jumaosi ya sikukuu ya Laborday nchini marekani. P-Unit wako USA kwenye Ziara yao ya mwezi mmoja ya "YOU GUY USA TOUR"

Kosura a.k.a Black Sugar akipata ukodaki na P-UNIT
MTANZANIA AJ UBAO akiwarusha Mashabiki na Kibao chake cha "WEWE" ambacho kiliwaacha wakina dada hoi nakulilia namba yake ya simu kwani wimbo huo unawagusa sana  mabinti.
AJ UBAO KATIKA MIONDOKO YAKE YAKIMASAI MASAI.
Picha hizi kwa hisani ya Vijimamboblog click for more