TAMASHA LA KISWAHILI (SWAHILI FEST) LILILOFANYIKA NCHINI MAREKANI NDANI YA WASHINGTON DC LAFUNIKA !

Kwa mara ya Kwanza kabisa nchini marekani limefanyka tamasha la Kiswahili katika jiji la Washington,likijumuisha nchi zote za Afrika Mashariki na kati zinazozungumza lugha ya kiswahili.Tamasha hili liliandaliwa ili kuweza kutangaza tamaduni za afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na Chakula,Mavazi,Ngoma za Asili,Miziki ya Kizazi Kipya,na mambo mbali mbali ya kiasilia.
Waandaaji wa Tamasha la Kiswahili Washington DC Ndugu Patrick Kajale na Dada Finiana wakijadili jambo na ndugu Safari ambaye ndiye Mtunzi wa kile kitabu Nambari moja Amazon cha Nyayo za Obama.
Ndugu Safari Akionyesha Kitabu cha Obama          Patrick Kajale  Mwandaaji wa Tamasha la Kiswahili
Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Mama Munanka akiwa amejumuika pamoja na watanzania waliofika kwenye tamasha hili la kiswahili.
Afisa  wa ubalozi wa Tanzania Dr Mkama akiwa na baadhi ya maofisa wa ubalozi.
Maofisa wa ubalozi wakiendelea kula nyamachoma kutoka katika banda la Safari Restaurant DC
Nyama Choma katika banda la Safari Restaurant Washington DC,Safari ni Mgahawa wa Kitanzania  uliopo katika jiji la Washington ambapo vyakula vingi vya kinyumbani vinapatikana.