SWAHILI MEDIA GROUP USA (MMK)-TUMETIMIZA SIKU TISINI !

TUMETIMIZA SIKU TISINISasa tunafikisha miezi mitatu tangu tuanzishe rasmi TV ,Blog na Radio online, kwa binadamu ni siku chache maana hata kutambaa atakuwa bado, kwa chombo cha habari  itategemea na uanzishwaji na wadau wake wanachukuliaje.

Kwa upande wetu tunachukulia bado tunakuwa, hivyo  tunamshukuru Mungu na wadau wetu  kwa siku hizi chache ambazo tumekuwa  hewani.

"Ni Jambo la kujivunia kwamba mmethubutu", tunanukuu maneno ya Waziri mkuu mstaafu mheshimiwa Edward Lowassa, aliyotueleza tulipofanya mahojiano naye hapa mjini Washington DC.  Tunaipokea kauli yake kwa unyenyekevu mkubwa na kama changamoto Kwetu sisi,wamiliki na wafanyakazi wote wa Swahili.

Ukubwa na nguvu ya chombo chochote cha habari unatokana na wadau ambao ndio wasikilizaji na wasomaji wake, nasi tunafurahia sana ushirikiano ambao Tumekuwa tukiupata kutoka kwenu nyinyi wadau wetu, tunapenda kusema hili kwa kudhamiria wasomaji na wasikilizaji wa Swahili Kwetu sisi nyinyi ni familia.

Tunapenda kuweka wazi kuwa bila ushirikiano wenu tusingeweza kufanya haya tunayoyafanya, licha ya muda huu mfupi tumeweza kufanikiwa kusogeza radio yako kwa karibu zaidi kwani sasa unaweza kusikiliza Swahili Radio kwenye simu yako ya kiganja (cell phone).

Katika kipindi hiki pia tumekuwa tukiwasiliana na wadau wetu ambao ni DCTV ili watukubalie show zetu tunazozalisha Kwao tuweze kuzionyesha kwenye online na pia Radio yetu iwe inasikika kwenye radio za kawaida hapa Marekani na Tanzania, tuko kwenye hatua za mwisho za kufanikisha hayo. Pia mikataba mbalimbali imeshafanywa ili kuanzia Novemba mpate vipindi mbalimbali na kwa muda maalum.

Tunawashukuru pia washiriki wetu VOA, BBC na Radio Umoja wa mataifa kwa  kushirikiana nasi na kukubali Swahili kurusha matangazo yao, hivyo kuanzia mwezi Novemba wadau wetu mtaweza kupata taarifa  za habari na vipindi mbalimbali kutoa katika radio hizo za kimataifa kupitia Swahili mtandaoni na kwenye simu za viganja.

Katika wingi kuna mengi,unapokuwa kwenye kusanyiko lolote lile kukwaruzana kupo, nasi kwa kutambua hilo, tunajua kuna sehemu nyingine tumekwaruza, tunapenda kusema samahani pale tulipokwaruza mtu au watu, kama waumgwana tunarudia kusema samahani na wale waliotukwaruza tumewasamehe, tunapofikisha siku  hizi tisini, Mbiu yetu ni "tufungue ukurasa mpya kwa maendeleo ya wote".
Tunakaribisha maoni na ushauri wenu, kama tulivyosema awali, nguvu yetu ni nyinyi wadau wetu, hiki ni chombo chenu, tunaahidi kuwa jicho, sikio na mdomo wa jamii, bila woga tutaripoti kwa nia ya kuhabarihisha, elimisha na kuburudisha lakini hatutotekwa na kiburi wala majivuno au woga, tunaahidi kuwa chombo huru cha habari lakini kinachojali maadili.

Pia tunakaribisha mtu yeyote anayependa kutoa ushauri au  kuhabarihisha ajisikie huru kuwasiliana nasi kwa email ya swahilimediausa@gmail.com, nasi tunaahidi kuwasiliana naye au kufanyia kazi ushauri wake au kupokea habari yake.
Kila siku ya ijumaa Swahili Blog itakuwa inatoa TAHARIRI.

NAY WAMITEGO ASEMA CHIDI BENZ AACHE KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA KAMA ALIVYOAHIDI!

               
                                                            NEY WA MITEGO
         
                                                              CHIDI BENZ
DROP BOX ni Segment (Kipengele) kinachopatikana kwenye kipindi cha DUNDO cha MJ FM kinachoendeshwa na DJ HAAZU ambacho kinampa nafasi Seleb mmoja kumzungumzia Star Mwenzake anavyomfahamu, vitu gani anavyovipenda kwake, vitu gani anavichukia na Ushauri wake kwake.

Amebananishwa Msanii anayefanya poa kwa ngoma yake ya Salamu zao na muziki gani "Nay wa Mitego" kumzungumzia Chid Beenz ambapo Nay aliamua kufunguka kwamba yeye ni Mmoja kati ya waliokuwa Mashabiki wakubwa sana wa Muziki wa Chid Beenz ila alimpoteza tu pale alipoanza kufanya mambo za ajabu ajabu ambazo kama ni Mtata utakuwa umegundua kuwa Kutoboa pua ni maja kati ya maajab ya Chid kwa Nay.
Nay anaamini kuwa mambo ya ajabu anayoyafanya Chid anashawishiwa na kutumwa na Madawa pamoja na Pombe zake na ndiyo maana pia anagombana na watu ovyo ovyo.

Kwa upande wa Vitu anavyovipenda hadi leo kwa Chid Beenz ni Flow yake na anavyoitune Sauti yake hapo ndipo Ney anaposema kuwa hata sauti yake inatokana kic kidogo na Sauti ya Chid kwani alikuwa anatamani kuwa kama Chid Kitambo hicho.

Ushauri wake ndo ukafikia hapo kuwa Chid aache Madawakama alivyoahidi kuwa anaacha na kusema kuwa kama angekuwa ameacha tungeona amebadilika.

MSIKILIZE NAY HAPA AKIFUNGUKA KWENYE DROP BOX 

EXCLUSIVE INTERVIEW -OMMY DIMPOZ ALONGA NA AYO TV DAKIKA CHACHE BAADA YA KUTUA BONGO !

Ommy Dimpoz alizungumzia kuhusu Mapokezi yake yalivyo kuwa,Jinsi Show zake zilivyo kuwa ikiwa ni pamoja na tofauti ya malipo kati ya show za nyumbani na za nje,Pia Brand yake ya nguo ya "PKP"
Hapa Dimpoz akiwa Washington DC akielekea Airport akionyesha Brand yake ya "PKP"
Hapa Dimpoz Akiwa Ndani ya Business Class akielekea Bongo
Baada ya kufika TZ angalia jinsi Kofia zake zilivyopata Fans kwa kasi
Hizi ni baadhi tu ya Kofia..kwa Kuoda Mpigie Mubenga !

Sikiliza Interview yake aliyo fanya na Millard Ayo wa AyoTV


SKYLIGHT BAND NDIO WAKALI WA TOWN, TUKUTANE THAI VILLAGE MASAKI LEO JIONI

IMG_0005  
Aneth Kushaba AK 47, Mary Lucos na Sam Mapenzi wakitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
IMG_0006
Mashabiki wa Skylight Band wakijiachia kwa raha zao.
IMG_0016
Mwanadada akionekana kuchuzika na Skylight Band...Hapana chezea kabisa...

WAJUE WALIMU WA KISWAHILI WASHINGTON DMV!


Mwalimu Mkuu wa darasa la Kiswahili. Mwl. Mkumbuka akipata picha ya pamoja na Mwl. Iris Zielske mara baada ya kusaini mikataba ya kufundisha watoto wa Kitanzania kwenye darasa la Kiswahili, DMV pale College Park, Maryland mapema wiki iliyopita.
               
Walimu  wa darasa la Kiswahili wakipata picha ya pamoja katika maandalizi ya kufunguliwa kwa darasa la Kiswahili, darasa lianaoratibiwa na Jumuiya ya Watanzania hapa DMV. Kutoka kushoto ni Mwalimu Bernadeta Kaiza, Mwl. Iris  Zielske,   Mkuu, Lucia Mkumbukwa, na Mwl Asteria Hyera. Darasa yatafunguliwa siku ya Jumamosi Oct. 19, 2013, saa tisa (3:00pm) pale University of Maryland, College  Park. Walimu Asha Nyang'anyi na Mama Anna Mukami (hawapo pichani) hawakuhudhuria mkutano huo.

Wakiwa na nyuso za furaha ni walimu wa darasa la Kiswahili hapa DMV mara baada ya mkutano wao ulioweka mikakati ya namna ya kuliendesha darasa hilo kwa ufanisi. Kutoka kushoto ni Mwalimu Mkuu, Lucia Mkumbukwa, Mwl. Bernadeta Kaiza, Mwl. Asteria Hyera na Mwl. Iris  Zielske ambaye ni mwalimu mpya kabisa  aliyejiunga na madarsa ya Kiswahili mwezi huu.