FAY DESTINY APATA USHINDI KWENYE TAMASHA LA KIMATAIFA LA MUZIKI WA INJILI MAREKANI.

                 1371356_10200791039954422_687147133_n
  1383470_10200554420324634_318863772_n
Fay Jukwaani. Mwanamuziki wa Injili anayeibukia miongoni mwa Watanzania hapa Marekani ni Bibie Fay Makame Haji a.k.a Fay Destiny mwanadada huyu mwenye asili ya visiwani Zanzibar, ambaye pia alibadili dini kutoka Uislam na kingia Ukristo alishiriki hivi karibuni kwenye mashindano ya uimbaji wa nyimbo za Injili wa kimataifa kwa nchi za Afrika katika jiji la Maryland na kufanikiwa kunyakua nafasi ya tatu ambapo alikumbana na washindani kutoka nchi nyingine mbali mbali za Afrika zikiwamo Nigeria, Liberia, Ethiopia,Sierra Leone n.k. Fay ameshatamba sana na kibao chake kiitwacho Inuka na nyimbo mbali mbali na baada ya kupepersha vyema bendera ya Tanzania kwenye michuano hiyo pia Fay alipata nafasi ya kufanya mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika (VOA) hapa Washington Dc na kusikiliza mahojiano hayo bofya hapa. [audio http://sundayshomari.files.wordpress.com/2013/10/mahojiano-na-fay-destiny.mp3] Wakati huo huo Fay Destiny anatarajia kuzindua albam yake ya kwanza Jumamosi huko katika ukumbi wa Hmpton Inn Hotel siku ya Jumamosi Oktoba 5,2013. ambapo atasindikizwa na wanamuziki kadhaa wa Injili wakiwamo kundi maarufu la JJ Sisters, Pastor Baraza na wengineo.Msikilize hapa akitoa habari hiyo kwa ukamilifu.