Tamasha Hili la "FEST AFRICA" hufanyika kila mwaka katika Jiji la Silver Spring ambapo Mwaka huu Tanzania iliwakilishwa vyema kama inavyooneka na Bendera ya Tanzania ikiwa ya Kwanza kabisa mkono wa kulia.Tamasha hili lilifanyika Jumamosi na Jumapili katika Viwanja vya Veterans Plaza Silver Spring jumapili kama inavyoonekana kwenye picha ndio ilikuwa siku yenyewe haswa.Mbali na Chakula cha Kiafrica ambacho hupatikana kwenye tamasha hilo,pia Mitindo ya Mavazi ya kiafrica pamoja na utamaduni na muziki wa kiafrica na ngoma za asili huonyeshwa.
LORRAINE KLAASEN akiwajibika jukwaani huku watu wakirikaruka bila kupata nafasi ya kukaa chini kwa masaa yote mawili aliyokuwa Jukwaani.
Emmerson Mwanamuziki kutoka Sierra Leone akitumbuiza kwa madaha kabisa akijivunia Uafrica wake ndani ya Marekani.
Kikundi cha Ngoma za Asili kikitumbuiza
Mwanadada Naomi kutoka Cameroon alikonga nyoyo za watu.
Mitindo ya Mavazi ya Kiafrica iliwarusha roho maelfu ya watu waliojitokeza huku mamodel wa Kiafrica wakizidi kujichukulia Umaarufu katika Jiji la Washington nchini Marekani.