SUGU APIGANA MBUNGENI.....JE IMEKAAJE???

Picha ya Mheshimiwa Mbilinyi akipigana Bungeni inazungumza mara           milioni  moja zaidi ya maneno  
 
                                   
                                                  MOHAMED MATOPE
Kwenye kampeni ya uchaguzi wa  raisi wa Amerika mwaka 1988 kulikuwa na mgombea mmoja anayeitwa Senator Gary Hart .Senator Hart wa steti ya Kolorado,  alikuwa  kijana anayevutia sana,mtu mwenye akili kupita kiasi ,mwanasheria aliyebobea na aliyeitumikia  serikali kwenye nyadhifa nyingi. Senator Hart alikuwa anaongoza kwanye kura za maoni kabla picha yake haijatolewa kwenye gazeti akiwa amekaliwa mapajani na mrembo (model) Donna Rice,ambaye alikuwa ni kimada wake.Ilichukua usiku mmoja kwa Senator Hart,kuporomoka kwenye kura za maoni ,kutoka asilimia thelasini na mbili mpaka asilimia kumi na saba.


Picha ya mgombea mweshmiwa Mheshimiwa Joseph Mbilinyi (Sugu),iliyotolewa magezitini akiwa amenyanyuliwa miguu juu,  na askari wa bungeni inamadhala sawa na ya Senator Gary Hart.Muheshimiwa Mbilinyi sio kiongozi wa upinzani,na pengine hatokuwa mgombea wa uraisi wa upinzani, hiyo inaelewaka dhahiri.Lakini jambo kubwa ni kwamba, Mh. Mbilinyi ni mbuge wa upinzani,kwa hiyo jambo lolote anolofanya , zuri au baya linaathili upinzani wote nchini.


Naelewa sio fair kwa kosa la kiongozi mmoja wa upinzani, liwaathili wapinzani wote,lakini ,binadamu ndio tulivyoumbwa ,tunajaji jumuia yote kwa kosa la mwanajumia mmoja.Na kwenye  siasa  kukumbanisha wapinzani wako pamoja ni mchezo wa kawaida.


Picha ya Muheshimiwa Mbilinyi ,italeta madhala makubwa mawili kwenye upinzani.Lakwanza, ni imevunja IMANI ndogo wanachi waliokuwa nayo kwenye upinzani.Ukiangalia uchaguzi wa uraisi wa mwaka 2000,2005 na 2010 ,wanachi wengi waliipigia kura  CCM, kwasababu ni chama ambacho wanakifahamu, kimewaongoza kwa muda mrefu,ndio,hawana raha nacho sana, lakini wanakiamini kwasababu wanakielewa.


Ni sawa na kuendeshwa baharini na kapteni wa meli ambaye amekuaendesha wewe na familia yako miaka zaidi ya hamsini,bila ya kukuzamisha baharini na kukuua. Unapoamua kumuajiri kapteni mpya jambo la kwanza utataka kufanya ni kumuelewa huyo kapteni mpya ili ujenge uaminifu juu yake.Picha ya mheshimiwa mbilinyi itawafanya wananchi wajiulize mara mbili,je tanawaamini wapinzani kutosha kuwakabidhi usukani  wa meli watuendeshe baharini kwa miaka mitano bila kutuzamisha?


kama leo wanapigana wakiwa ndani ya Bunge , je tukiwapa uraisi si watauwana ndani ya Ikulu


Jambo la pili picha ya Muheshimiwa Mbilinyi ilichofanya ni ,imewalaisishia kazi CCM kwenye kampeni ya 2015. Imewapatia CCM advertisement ya bure. Kama CCM wataitumia hii picha  ya Muheshiwa Mbilinyi kiuharisi ,na kuionyesha  katika kila kona ya nchi, kwanye TV,matangazo na mabango ,na kuwauliza wananchi  swali moja tu ,ndio hata kama mmechoka na sisi, hata kama hamtupendi, je mpo tayari kuwakabidhi serikali yenu tukufu  watu kama  hawa? Na kama CCM wataweza kumuunganisha Mh. Mbilinyi na wapinzani wote kwenye boxi moja, case closed! Uchaguzi utakuwa umeisha.


Mwalimu Nyerere alituhusia kuwa Ikulu ni mahari patakatifu,na kama Ikulu  ni mahari patakatifu,basi utakatifu unaanzia bungeni. Maraiisi wetu wote waliotawala nchi yetu wametokea bungeni.Vile vile,bunge linatunga sheria za nchi,na watanzania wengi leo wanatumikia vifungo kwenye majela kwasababu wamevunja sheria zilizotungwa  na bunge,kwasababu hiyo, tunawashikilia wabunge wetu kwenye standadi ya juu.


Senator Hart, alitumia wiki nzima kujielezea ,na kuomba misamaha ya kila aina,lakini haikusaidia, mwishowake akaliondoa jina lake kwenye kugombea uraisi.Labda Muheshimiwa Mbilinyi anao ufafanuzi mzuri wa mambo yaliyotokea bungeni kabda hajanyanyuliwa kichwa chini miguu juu na polisi wa bunge,na pengine hakuvunja sheria yeyote ya nchi.Naibu Spika alishamsamehe,na amemruhusu kurudi bungeni ,hana sababu yeyote ya kujiuzuru kama senator Hart, lakini  (damage is done ) picha inazungumza mara milioni moja zaidi ya maneno.
Mwisho.


Mohamed Matope ni mwandishi wa blogu mbalimbali za Tanzania na Afrika.