DIAMOND PLATNUMZ AFANYA MAKAMUZI YA NGUVU KANSAS CITY, MISSOURI NCHINI MAREKANI

Diamond Platnumz prezda wa wasafi akifanya makamuzi Kansas City siku ya Jumapili July 6, 2014 katika kukamulisha sherehe za uhuru wa Marekani  onesha lake likihudhuriwa na mashabiki wa Afrika Mashariki wakiwemo wazawa kibao waliojitokeza kumuunga mkono.
Diamond Platnumz akiendelea na makamuzi ndani huku akiwa amezungukwa na mashabiki wa Kansas City na wenggine wakiwa wamesafiri kutoka majimbo ya jirani.
Mashabiki wa Diamond Platnumz wakicheza pamoja nae wakati prezda wa wasafi akiendelea kufanya makamuzi ya nguvu ndani ya Kansas City, Missouri.
Diamond Platnumz akiendelea kufanya makamuzi ya nguvu ndani ya Kansas City MO mashabiki wengine wakipata picha mbili tatu na wengine wakiwa wanarekodi video.
Prezda na madansa wake wakiendelea kulishambulia jukwaa Kansas City.
Mashabiki wa Diamond wakiwa wamechanganyikiwa Prezda mwenyewe akiendelea na makamuzi ya nguvu.
Mashabiki kama unavyoona kwenye picha wakitaka japo wamguse prezda wa wasafi kwenye show yake ya Kansas City aliyofanya siku ya Jumapili July 6, 2014 na kuhudhuriwa na mashabiki kila kona ya Missouri na Kansas na wengine wakiwa wamekuja toka majimbo mengine ya jirani
Mashabiki wa Diamond Platnumz wakiendelea kupagawa. Kwa picha zaidi bofya HAPA

DIAMOND PLATNUMZ ATINGA MDANI YA STUDIO ZA GENN ONLINE RADIO

Mashabiki wa Diamond Platnumz wakipata nae picha ya pamoja na Rais huyo wa Wasafi alipokuwa akiwasili kwenye mji wa Olathe jimbo la Kansas ilipo Radio hiyo ya GENN kwa mahajiano kabla ya show yake inayotarajiwa kufanyika muda si mrefu katika anuani ya 8625 Troost Ave, Kansas City, Missouri.
Mtangazaji wa GENN Radio AJ (mwenye kofia nyeusi wapili toka kulia) akimfanyia mahojiano Diamond Platnumz ndani ya Studio ya Radio hiyo ambayo inapatikana mtandaoni www.gennmedia.com wengine ni Dj Romy Jons Poromota DMK na Dj Bston (kulia) 

ANOTHER HIT FROM DIAMOND..NEW "MDOGOMDOGO

BRAND NEW FROM DIAMOND " BUM BUM"