MISSY TEMEKE AWASILI CALIFORNIA SALAMA SALMINI-READY FOR SUMMER OF LOVE FASHION SHOW !

                 
               DRESS BY KWETU FASHION-DESIGN YAKE MWENYEWE MWENYEWE
                    
                                               HAYO MABEGI SASA DUH !

VIDEO-VANESSA MDEE "ME & YOU"

MHE. ALI HASSAN MWINYI MGENI RASMI,MASANJA, SHILOLE KUFANYA MAKAMUZI MIAKA 3 YA VIJIMAMBO NA TAMASHA LAUTAMADUNI WA KISWAHILI MAREKANI

Blog ya Vijimambo ikishirikiana na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini, Washington, DC, Marekani na Jumuiya ya Watanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia wanapanga kusheherekea miaka 3 ya Vijimambo na kukuletea tamasha ni kuendeleza lugha na utamaduni wa Kiswahili hapa Marekani ili watoto wanaoishi huku waweze kuendeleza matumizi ya lugha hii na utamaduni wake kizazi hadi kizazi. 

Siku ya July 6, 2013  hapa DMV kwenye Hall la Hampton Conference Center lililopo 
207 w Hampton Pl, 
Capitol Height, MD

Mambo mengi yatakuwepo, Vikundi mbalimbali vya utamaduni, wanamitindo ya mavazi mbalimbali kuwakilisha, vyakula vya Kitanzania, Wasanii kutoka nyumbani Shilole na Masanja wakishirikiana na hapa Marekani yote ni kudumisha utamaduni wetu wa kiswahili
HOTEL KWA AJILI YA WAGENI
Tumeongeza vyumba 35 Hotel ya Country Inn & Suites 
Na unapopiga simu uliza SWAHILI CULTURE IN USA kusudi upate unafuu wa bei nambari ya simu ni 301 350 8088 na Addrees ni
8850 Hampton Malls Drive North
Capitol Heights, MD 20843

Hotel za jirani na hapa ni
Hampton Inn
9421 Largo Dr West,
Largo, MD 20774
simu ni 301 499 4600

Extended Stay American

9401 Largo Drive West,
Largo, MD 20774
simu ni 301 3339139

Confort Inn
56 Hampton Park Blvd
Capitol Heghts, MD20743
Simu ni 301 336 8900
-------------------------------------------------------
kwa wajasiriamali ambao wangependa kudhamini na kuijipatia meza ya kutangaza bidhaa au shughuli wazifanyazo tafadhali wasiliana 301 613 5165301 661 6696 na 301 792 8562mwisho ni June 15, 2013 Asante

MSANINI MAHILI WA HIP HOP "LANGA" AFARIKI DUNIA KWA MALARIA KALI YA UTI WA MGONGO !
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Langa Mengisen Kileo, leo jioni amefariki katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar baada ya kuugua malaria na kisha kujitokeza homa ya uti wa mgongo.
Akizungumza na matandao wa GLOBAL PUBLISHER, baba mzazi wa Langa, Mzee Mengesen Kileo, amesema alimpeleka mwanaye Hospitali ya Kinondoni maarufu ‘Kwa Dokta Mvungi’ ambapo aligundulika kuwa na malaria na baadaye aligundulika kuwa na homa ya uti wa mgongo. Mzee Mengisen aliongeza kuwa, baada ya Dokta Mvungi kugundua kuwa Langa ana homa ya uti wa mgongo ambayo ni hatari, leo asubuhi aliamua kumkimbiza hospitali ya Muhimbili na kumfikishia chumba cha wagonjwa mahututi ‘ICU’. Baba huyo wa marehemu alizidi kuueleza mtandao huu kuwa, ilipofika mida ya saa kumi jioni, mwanaye aliaga dunia. Mipango ya mazishi inaendelea kupangwa nyumbani kwao marehemu Mtaa wa Chato, Mikochocheni jijini Dar.
MUNGU  AILAZE ROHO YA MAREHEMU PEPONI !!