P SQUARE LIVE IN WASHINGTON DC ..JUMAMOSI YA SEPT 5 .....NUNUA TICKET YAKO MAPEMA !!


AISHA YAZINDULIWA KWA KISHINDO WILAYANI PANGANI

1- moja
Filamu iliyopewa jina la AISHA imezunduliwa rasmi siku ijumaa ya tarehe 31/7/2015 wilayani Pangani chini ya shirika lisilo la kiserikali la UZIKWASA.
Aisha ni filamu ya tatu katika mfululizo wa filamu za UZIKWASA zikiangazia aina mbali mbali za unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto wa kike. Filamu hizi ni ni sehemu mojawapo tu ya njia za mawasiliano katika kampeni shirikishi-jamii ya mabadiliko ya tabia inayofahamika kama 'BANJA BASI'!, Pangani, Tanga.
Kabla ya filamu ya Aisha iliyozinduliwa kwa kishindo hivi karibuni, shirika la UZIKWASA tayari limeshatengeneza filamu nyenigne mbili ambazo ni FIMBO YA BABA na CHUKUA PIPI, wengi wa waigizaji waliomo ni wasanii wa vijijini.