KHADIJA KOPA AMSHUSHUA MWIZI ALIYEMWIBIA GARI LAKE KWA KUMTUNGIA WIMBOMalkia wa mipasho nchini Khadija Kopa ameamua kuzielekeza hasira na uchungu wa kuibiwa gari lake kwa kutunga wimbo kumshushua mwizi wa gari hilo.
Wimbo huo uitwao ‘Mjini Chuo Kikuu’ mwanzo mwisho umeandikwa kumponda kibaka huyo aliyemharibia mipango yake ya kifedha kwa kumlazimisha kufikiria kununua gari jingine.
Gari la Khadija Kopa lenye thamani ya shilingi milioni 15 liliibiwa mwezi uliopita.
Jumla ya magari manne yaliibiwa likiwemo gari la msanii wa kizazi kipya Nyandu Tozi maarufu zamani kwa jina la Dogo Hamidu aina ya Vits ya silver ya 2002 T698 BUH.
Magari hayo yaliibiwa siku moja mahali yalipokuwa yameegeshwa karibu na shule ya Mwananyamala B.
Kwa mujibu wa tovuti ya Milard Ayo, mpaka sasa magari yote hayajapatikana ambapo magari manne yaliyoibwa kati ya 18 yaliyokuepo kwenye eneo hilo.