JAMBO SQUARD, WARRIORS FROM THE EAST, JCB NA JOE MAKINI WASEMA WASANII WA ARUSHA WAMEDHARAULIKA NA KUNYIMWA HAKI YAO YA KILI MUSIC TOUR
Jambo Squards Wakiwa na Producer DX na ile tuzo yao ya kundi bora la mwaka
Kupitia MTAA WA PILI ROUND II ya Mambo Jambo Radio Arusha 93.0 FM na DJ Haazu amepiga story na Wasanii walioshinda tuzo kupitia Kili Music Awards 2013 kutoka Arusha ambao ni Jambo Squard ambao walishinda tuzo ya kundi bora la mwaka na Warriors From the East walioshinda Tuzo ya wimbo bora wa Reggae kwa mwaka 2012-2013 Kupitia Kili Tanzania Music Awards ambapo kikubwa alitaka kujua kuhusu Kili Music Awards Tour ambayo imekamilika juzi Dar Es Salaam ambapo Wasanii hao wamepata kufunguka kuwa Kili Music Tour imewadharau.
WARRIORS
Hii inatokana na Mshangao Mkubwa ambao kila Mtu ameupata baada ya kujua kwamba Wasanii hao pamoja na kuchukua Tuzo kwenye Tour ya Kuzionyesha tuzo na kuwashukuru Mashabiki waliowapigia kura Imeonekana wazi wao wakibaguliwa na hatimaye kutoitwa Kwenye tour nzima badala yake wao kuhusika tu kwenye Show ya Kili tour pale Kilimanjaro ambapo yenyewe hawakuwekwa official bali wao kung'ang'ania na kupewa show ile moja ambayo wao wanaiita ya kufuta aibu flani kwani hata kwenye matangazo ya Promo hawakutajwa. Wanachokilalamikia wao ni kunyima ziara ambayo ndiyo ambayo ingewapa chochote kile na badala yake Wasanii ambao hata hawakuchukua tuzo na wengine ambao hata hawakuwa Categorized lakini wamezungushwa katika karibu tour nzima na kula kwa migongo yao. Wasanii wote Jambo Squards na Warriors wameonewa na Wao kufunguka kuwa Wasanii wa arusha Wanadharauliwa na Kubaniwa na ndo maana pia hawapewi nafasi ila wao wamesema harakati zinaendelea. Kili music Awards Tour mwanzoni ililetwa na Swagger za Washindi wa Awards kwenda kuwashukuru Fans kwa Kura kitu ambacho kinaonekana kimeendewa kinyume na maumbile yake.
HIKI NI KIPANDE TU CHA VIDEO WAKATI JAMBO WANAPAGAWISHA MASHABIKI KWENYE KILI MUSIC TOUR 2013 PALE MOSHI MABAYO WANASEMA WALIPEWA NAFASI KIMAZABEZABE ANGALIA VIDEO HAPO CHINI
Haazu amepata piga story pia na JCB na Joe Makini wamepata kustick pale pale kuwa ni kweli Wasnii wa Arusha Wamezaraulika na kushusshwa thamani na waandaaji wa Kili Music Tour kitu ambacho wao wamekichukulia kuwa sio haki.
Joh Makini
JCB & JOE MAKINI wamepata kufunguka kiundani sana na kusema kuwa hizi Tuzo zimejaa ududu sana na watu wanapeana Tour kwa kujuana na kishkaji wakati wao wanauwezo wanabaniwa.
JCB anasema wakisema ukweli wanasema eti tunaTabia Mbaya
Huu umeonekana kama uovu wa Tuzo hizi ambazo pia zimekuwa zikilalamikiwa na Wasanii wengi sana na Habari hii ina mwendelezo na kifuatacho utasikia walichojibu Waandaaji wa Kili Music Tour Fuatilia hapa hapa.
FULL INTERVIEW YA DJ HAAZU, JAMBO SQ., WARRIORS FROM THE EAS, JCB NA JOE MAKINI HII HAPA CHINI SIKILIZA.
KUSIKILIZA INTERVIEW CLICK HAPA
LINK YA SAUTI http://www.hulkshare.com/wxj8fzxr0idc
Subscribe to:
Posts (Atom)