BONGO MOVIE TUTAFIKA KWELI???


   Kweli Bongo Movie Tutafika kweli??
Mwanadada Irene Uwoya amepost Picha hii kwenye Instagram yake akionyesha kuwa alikuwa Location akishoot Movie.Tatizo ni kwamba katika picha hiyo inamuonyesha jambazi aliyemvamia Irene nyumbani kwake lakini kabla ya kuvamia alivua Viatu.
   Je tangulini jambazi akaogopa kuchafua nyumba aliyoivamia,Director wa Movie hii ni nani?????

LUCCI KUDONDOSHA "SUMU" YAKE TAREHE 13 OCTOBER!


Ikiwa ni takribani mwezi mmoja umepita toka producer wa audio wa studio ya Transformax, Luciano Gadie Tsere maarufu kama Lucci aachie video ya duet yake na mrembo Jokate Mwegelo ‘Kaka/Dada’, producer huyo anategemea kuachia video mpya ya wimbo unaoitwa ‘SUMU’. Director Nisher ambaye jina lake linaendelea kukua kutokana na kazi anazoendelea kufanya ndiye aliyehusika kuandaa Video hiyo ya SUMU.Kama Flyer hiyo inavyoonyesha Siku moja tu imebaki.Tembelea hapa kesho kujionea mwenyewe hiyo SUMU.

FROM NIGERIA "P-SQUARE SASA KUTUA BONGO NOVEMBER 23!

002.JP

004.JP
    Mtangazaji wa East Afrika Radio, Hillary Daudi (Zembwela)akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza ujio wa wasanii wa muziki wa kizazi kipya Peter na Paul Okoye maarufu kama  P – Square  kutoka nchini Nigeria pamoja na mdhamini Mkuu,Tarehe 23 Mwezi ujao ndipo watawasili nchini. Wasanii hao wataambatana na wasanii wengine 13 kutoka nchini humo. Pamoja nae katika Picha ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasilino wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa ambo ndio wadhamini wa onesho hilo.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt jijini Dar, Hillary Daudi wa East Afrika Radio, Amesema onesho hilo litakuwa la kipekee. P- Square wataongozana na wasanii wengine 13 ambao watatoa burudani ya Live Band siku hiyo Pamoja na wasanii wengine kutoka Tanzania.Wote tunatambua namna kundi hili linavyofanya vizuri ndani na nje ya bara la Afrika, licha ya kutoa burudani kwa mashabiki, pia litatoa fursa kwa wasanii wa ndani kujifunza kutoka kwa wasanii hawa vijana ambao wamepata mafanikio makubwa kutokana na kazi yao ya muziki,” alisema na kuongeza “hii itakuwa ni fursa ya kipekee kwa wasanii wetu wa bongo kujifunza kwa kuangalia wenzao wanavyofanya kazi”. Tutaendelea kuwaletea Habari zaidi za tour hiyo.