WEMA SEPETU AWASHINDA POLICE WALIOKUJA KUMKAMATA BAADA YA KUPIGA MUZIKI KWA SAUTI YA JUU USIKU NA MAJIRANI KUITA POLICE!

Habari Hii na Global Publisher :Imethibitishwa na DMK411
                              MSANII WA FILAMU WEMA SEPETU
Katika hali ya kushangaza, polisi walijikuta wakipata shughuli pevu kumkamata staa asiyeishiwa matukio Bongo, Wema Sepetu ambaye alidaiwa kupiga muziki kwa sauti kubwa usiku kucha pasipo kuwa na kibali, Amani linakupa mchapo.
Timu iliyofika nyumbani kwa Wema Sepetu kumkamta kwa usumbufu aliosababisha kwa majirani.
Tukio hilo lilitokea Jumanne iliyopita, nyumbani kwa mwigizaji huyo, Kijitonyama jijini Dar kulikokuwa na bethidei ya rafiki yake aliyejulikana kwa jina moja la Neema.
Awali, mapaparazi wetu walipokea simu ya mmoja wa majirani wa Wema ambaye alidai mwigizaji huyo amekuwa na tabia ya kufanya sherehe kwake na kufungulia muziki mkubwa ambao unasababisha kero.
Spika na vifaa vingine vya muziki vilivyotumika katika sherehe hiyo vikiwekwa kizuizini.
“Kwa kweli ni kero, kila mara amekuwa na tabia ya kupiga muziki mkubwa katika sherehe zake ambazo hazina kichwa wala miguu. Kama jana (usiku wa Jumatatu) muziki ulifunguliwa kuanzia saa mbili usiku mpaka asubuhi na majirani walimfuata Wema mara kadhaa kumtaka apunguze sauti lakini aliwajibu vibaya.
Polisi akisimamia zoezi hilo kwa kuwawajibisha wahusika (mmiliki wa muziki na mwenye sherehe).
“Njooni mshuhudie wenyewe, tumeita polisi wamkamate,” alisema jirani mmoja.
Mapaparazi wetu walichukua usafiri wa pikipiki na kuwahi fasta na kukuta polisi wakihangaika kwa muda mrefu kumkamata mrembo huyo lakini ikashindikana kwa kuwa alikuwa amelewa na kukimbia hovyo huku akiwa nusu utupu.
Mwenye sherehe, Neema( rafiki wa Wema Sepetu) akichukuliwa kwenye bajaji.
“Kwa sababu hiyo walimkamata mmiliki wa muziki ambaye jina lake halikupatikana mara moja na mwenye sherehe (Neema) kisha kwenda nao katika ofisi za mtendaji, Kijitonyama  kwa ajili ya hatua za kisheria,” alisema.

DANCER WA DIAMOND "MOSES IYOBO" AFUNGUKA -ASEMA MIMBA YA BABY WAKE STAR WA FILAMU AUNTY EZEKIEL NI FARAJA KWAKE!


MOSES IYOBO nambari one Dancer wa  Nasibu Abdul  ‘Diamond’ amefunguka kuwa hakuna kitu kinachompa faraja kubwa kama mimba ya mpenzi wake ambaye ni staa wa filamu Bongo, Aunty  Ezekiel.
Mimi tu nikiwaza mtu ambaye ninampenda kwa dhati ana mimba yangu napata faraja kubwa sana hivyo kila siku namuomba Mungu ajifungue salama na ampitishe katika majaribu mazito,” alisema Iyobo.

SAFARI RESTAURANT-CHAKULA CHA KITANZANIA-KWA WATANZANIA NA MATAIFA YOTE- KARIBUNI !
                

VIDEO- DIAMOND ALIVYOWARUSHA WANA DAR PALE TIGO KIBOKO YAO !

BREAKING NEEEEEEWWZZZZ - JE NI MSANII GANI ATAKAYE WARUSHA ROHO KWENYE BIRTHDAY BASHH YA CCM NEW YORK FEB 21?????..NUNUA TIKETI USIJE JILAUMU -DETAILS DROPPING SOON !

Hii itakuwa ni Sherehe ya aina yake kufanyika katika Jiji la Wajanja Big Apple,Watu wote bila kujali Itikadi zao wanaalikwa kwani hii ni Birthday Bashhh na sio mkutano wa kisiasa,Njoo uburudike na watanzania wenzako kutoka states mbali mbali pamoja na Nje ya nchi,kutakuwqa na Burudani kutoka kwa wasanii maarufu kutoka Tanzania,Habari zaidi za Wasanii na Mgeni Rasmi kufuata.
                                                   Tuungane Tuiline Tanzania Yetu                          

                                         UKUMBI WA RICHI RICH PALACE KWA NJE                          
                                     UKUMBI UNAVYOONEKANA KWA NDANI
                          
                                                  TICKETS PRICE: ADVANCE $40 | DOOR $50
Inclusive of:
Red Carpet Grand Entrance
Photo up Dress Ready
*3-Course Dinner
*Soft Drinks
*Elegant Settings
*Live Entertainment
*Cash - Bar Beer $3| Liqour $5 | Wine $5 | Patron $7
CALL: 347-663-0781  | 917-698-6943