KIJIWE CHA UGHAIBUNI KUWA HEWANI JUMANNE JULY 23, 2013

 Kipindi chako ukipendacho cha Kijiwe cha Ughaibuni kitaanza kurushwa tena kuanzia Jumanne wiki ijayo July 23, 2013 kipindi hiki kilisimama kutokana na pilikapilika ya sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la utamaduni wa Kiswahili Marekani. Vijimambo inaomba radhi kwa wadau na masahabiki wa kijiwe cha ughaibuni kwa usumbufu wowote uliojitokeza kwa kutorusha kipindi hiki.
 Juu na chini ni kruu nzima ya kijiwe ikitafakari jambo

CHAMELEON AACHA HISTORIA CALIFORNIA KWA MIONDOKO YAKE NA MTANZANIA ERICA NAYE ALIFUNGUA PAZIA KWA KISHINDO!    Hapa mwanamuziki huyo kutoka UGANDA akiimba hit song yake "VALU VALU" wimbo ambao ulimpatia tuzo za Kilimanjaro nchini tanzania kama Wimbo bora wa mwaka 2013.


DR JOSE CHAMELEON BAADA YA KUPIGA SHOW DC..alielekea California ambapo mbali na ustadi wake wa kuimba aliwaacha hoi washabiki wake kwa kucheza nao bega kwa bega.

 Hapa Chameleon anaonekana akiufeel Mchezo wa huyu dada wakati Bwana Walter Minja akiangalia kwa umakini zaidi pembeni yao.
                            Hapa sina lakuongea maana mabo yanajieleza yenyewe.  SHOW ilianza kwa Mwanadada Mtanzania aishie CALI "ERICA" kufungua show kwa kishindo.Erica ni Mtanzania anayefanya shughuli zake za Muziki hapa marekani na amekuwa akizunguka karibu nchi nzima akifanya show zake kwa umakini wa hali yajuu.Erica pia anatazamiwa Kufungua SHOW YA "OMMY DIMPOZ" atakapokuja Mwezi ujao huku akisindikizwa na mwanamuziki wa bongo Fleva aishie Washington DC "AJ UBAO"


               ERICA AKIWAPELEKA MASHABIKI WAKE MCHAKA MCHAKA.
                          PICHA KWA HISANI YA WATANZANIA KUTOKA BAY AREA.

KIBAO KIPYA-NYEMO "MAMACITA"

Baada ya kutoa vibao vyake viwili mwaka jana "DANI" na "MAMA" Mwanamuziki Mtanzania NYEMO SOUND OF AFRICA,Sana amekuja na "MAMACITA"...check Kideo yake hapo chini.