
Ndugu Dickson anayefahamika kwa wengi kama Mr "DMK "

Kampuni hii inafanya Shuguli zake Marekani za kuandaa Events mbali mbali za burudani kama CLUB EVENT,CONCERTS, CARNIVALS ikiwa ni pamoja na kuleta wasanii Marekani kutoka Tanzania na Africa kwa ujumla,pia inafanya matamasha ya Burudani na wasanii wa Marekani pia.Baada ya Tuzo hizi Tulimpigia simu bwana DMK na kumpongeza kwa kuiwakilisha vyema Tanzania na East Africa kwa ujumla ambapo aliwashukuru sana waliompigia kura kote Duniani na kuongezea kuwa Tuzo hii ameipata yeye lakini angependa ijulikanekuwa shughuli hizi huwa anazifanya kwa kusaidiana na Partners wake kampuni za Safari Entertainment na J&P Ent ambazo amesema kuwa bila wao kushurikiana nao asingekuwa hapo alipo.
Bwana DMK amesema tutegemee Mambo makubwa mengi kutoka kwake na Partners wake hivi Karibuni.