TAMASHA LA KISWAHILI (SWAHILI FEST) LILILOFANYIKA NCHINI MAREKANI NDANI YA WASHINGTON DC LAFUNIKA !

Kwa mara ya Kwanza kabisa nchini marekani limefanyka tamasha la Kiswahili katika jiji la Washington,likijumuisha nchi zote za Afrika Mashariki na kati zinazozungumza lugha ya kiswahili.Tamasha hili liliandaliwa ili kuweza kutangaza tamaduni za afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na Chakula,Mavazi,Ngoma za Asili,Miziki ya Kizazi Kipya,na mambo mbali mbali ya kiasilia.
Waandaaji wa Tamasha la Kiswahili Washington DC Ndugu Patrick Kajale na Dada Finiana wakijadili jambo na ndugu Safari ambaye ndiye Mtunzi wa kile kitabu Nambari moja Amazon cha Nyayo za Obama.
Ndugu Safari Akionyesha Kitabu cha Obama          Patrick Kajale  Mwandaaji wa Tamasha la Kiswahili
Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Mama Munanka akiwa amejumuika pamoja na watanzania waliofika kwenye tamasha hili la kiswahili.
Afisa  wa ubalozi wa Tanzania Dr Mkama akiwa na baadhi ya maofisa wa ubalozi.
Maofisa wa ubalozi wakiendelea kula nyamachoma kutoka katika banda la Safari Restaurant DC
Nyama Choma katika banda la Safari Restaurant Washington DC,Safari ni Mgahawa wa Kitanzania  uliopo katika jiji la Washington ambapo vyakula vingi vya kinyumbani vinapatikana.

TAMASHA LA KISWAHILI JUMAPILI HII-MAMBO YAZIDI KUPAMBA MOTO,VINOGESHO NA MATAIFA MBALI MBALI YAZIDI KUTHIBITISHA KUHUDHURIA.(WASHINGTON DMV)


MAYOR WA MJI WA BLADENSBURG KUHUTUBIA, MABALOZI WA NCHI ZA AFRICA MASHARIKI WATAKUWEPO,FREE BOAT RIDE KUZUNGUKA MTO, MICHEZO YA WATOTO, UTAMADUNI WA AFRIKA MASHARIKI,VENDORS,CHAKULA CHA AFRIKA MASHARIKI KUTOKA SAFARI RESTAURANT DC, VINYWAJI BARIDI VYOTE VINAPATIKANA:
                                                    HAKUNA KIINGILIO NI BUREEE!

BLOG YA VIJIMAMBO YAKABIDHI MCHANGO WAKE WA KUSAIDIA KUPAMBANA NA UJANGILI KWA MHE. LAZARO NYALANDU

Baraka Daudi, Mwenyekiti wa Tamasha la Utalii na kukemea ujangili lililoadhimisha miaka 4 ya Blog ya Vijimambo akimkabidhi pesa tasilimu $1,000 kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu kwa ajili ya kupambana na ujangili makabidhiano yaliyofanyika katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani siku ya Jumatatu Sept 15, 2014
Mhe. Lazaro Nyalandu, Balozi Leberata Mulamula Afisa Ubalozi Suleiman Saleh (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Vijimambo Baraka Daudi na Mayor Mlima baada ya makabidhiano ya pesa ya kupambana na Ujangili