OMMY DIMPOZ AFANYA VIDEO NA SUPER MODEL SOFIA SK WA JIJINI LONDON


 Mwanamuziki Mahiri kutoka Tanzania ambaye kwa sasa yuko London anashoot Video ya wimbo wake mpya,Akizungumza na Swahili Media Group amesema kuwa anayofuraha kuweza kufanya kazi na Supermodel anayetikisa jiji la London.Alipoulizwa na Mwandishi wetu je imekuwaje akaweza kumpata model huyo Dimpoz alitabasamu nakusema Siri yake na pia akasema Model huyo ni fan wake mkubwa pia
kwani anapenda sana miziki ya Dimpoz ingawa Kiswahili hajui.Dimpoz amewaomba wapenzi wake wakae mkao wakula kwani video hiyo itakuwa ni balaa.

                OMMY DIMPOZ NA SOFIA SKVORTSOVA KATIKA VIDEO SHOOT


MSIBA NEW YORK NA TANZANIA

Mtanzania mwenzetu Mama Lulu John Maro Mwaluko amefariki dunia asubuhi ya siku ya Ijumaa tarehe 7 Machi 2014. Mama Mwaluko alikuwa akikaa Queens, New York na alishawahi kuwa mwalimu na alifundisha high school hapa New York. Mama Mwaluko alifariki baada ya kuugua ugonjwa wa saratani yaani kansa. Alikuwa akitibiwa huko katika hospitali ya Calvary huko Bronx, New York.

Mama Mwaluko alishawahi kukaa na Marehemu mumewe China na Marekani kama Wanadiplomasia na alishastaafu kufundisha mwaka 2012 na kabla ya kufariki alikuwa mbioni kurejea Tanzania.

Mama Mwaluko atakumbukwa na familia yake kama mama, dada, shangazi, mwalimu, mcha Mungu na mama mwenye busara. Katika kuomboleza msiba wa Mama Mwaluko, Watanzania wote tunaombwa kuifariji familia yake na ndugu zake kwa kujumuika nao katika sala na michango katika wakati huu mgumu wa maombolezo. Taarifa zaidi zitafuata baadae lakini kwa sasa mnaweza kuwasiliana na 

Emma Kasiga kwa simu namba 
612-229-4050 
 Nanna Mwaluko kwa simu namba 
347-693-6129 
na Camelot Funeral Home kwa simu namba 
914-664-8500.
 Taarifa zaidi za msiba huu zitafuata baadae.

Siku ya Jumatano itakuwa ni siku ya kuaga mwili wa Marehemu kuanzia saa tisa na nusu hadi saa mbili za usiku pale Camelot Funeral Home. Anwani ni: 

Camelot Funeral Home, 
174 Stephens Avenue, 
Mount Vernon, New York, 10550. 
Wote mnaombwa kufika kumuaga Mama Lulu John Maro Mwaluko na kuifajiri familia yake. Taarifa zaidi za utoaji wa michango ili kufanikisha msiba huu na rambirambi zitafuata baadae.


Mwenyezi Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amen.

Imetolewa na Uongozi - Jumuiya ya Watanzania New York.

Deogratius Mhella
The Executive Secretary
New York Tanzanian Community
c/o Tanzania Mission to the UN
307 East 53rd Street, 4th Floor
New York, NY 10022
Tel: 201-252-7220
Email: info@nytanzaniancommunity.org

KIJIWE CHA UGHAIBUNI



HOYCE TEMU AMONG TOP MISA'S WOMEN TO WATCH 2014

Picture-055
Hoyce Temu a communication specialist at the United Nations in Tanzania has been selected as one of the inspirational southern African women and a rising star in the region.
Temu has been involved in the social works by helping the communities in various ways and sharing what she has to make the world a better living for everyone.
On the International Women’s Day, the MISA announced the first annual MISA’s Women to Watch.
MISA is honoring 12 dynamic­­ and inspirational southern African women who embody both the official United Nations theme for International Women’s Day 2014 - Equality for women is progress for all – as well as the theme designated by non-governmental organisations around the world –Inspiring Change.
MISA Regional Director, Ms Zoe Titus said, “We chose women who we see as rising stars in the region, women whose achievements to date are a promise of more great work to come, making them women to watch.”