PICHA YA "LULU" MSANII ANYEDAIWA KUSABABISHA KIFO CHA "STEVEN KANUMBA"


Habari za muda huu zinaeleza kuwa Jeshi la Polisi limeanza kumhoji 'mtoto' anayeshukiwa kuwa chanzo cha Steven Kanumba (The Great), Elizabeth Michael, maarufu kwa jina la kisanii, Lulu, amekanusha kumsukuma msanii huyo nguli hadi kufa.Amesema kamwe hakufanya hivyo, pamoja na kwamba walikuwa wamekwaruzana kwa muda mfupi na akaenda kuoga, akiwa anatoka bafuni alianguka (aliteleza) na kugonga kichwa kabla ya kukutwa na umauti.
Binti huyo ameiambia Polisi kwamba Kanumba (ambaye wamekuwa na uhusiano naye wa mapenzi kwa muda sasa) alikuwa 'amebugia' ujazo mkubwa wa pombe kali aina ya Jack Daniels (JD). Uchunguzi bado unaendela.