LUCCI KUDONDOSHA "SUMU" YAKE TAREHE 13 OCTOBER!


Ikiwa ni takribani mwezi mmoja umepita toka producer wa audio wa studio ya Transformax, Luciano Gadie Tsere maarufu kama Lucci aachie video ya duet yake na mrembo Jokate Mwegelo ‘Kaka/Dada’, producer huyo anategemea kuachia video mpya ya wimbo unaoitwa ‘SUMU’. Director Nisher ambaye jina lake linaendelea kukua kutokana na kazi anazoendelea kufanya ndiye aliyehusika kuandaa Video hiyo ya SUMU.Kama Flyer hiyo inavyoonyesha Siku moja tu imebaki.Tembelea hapa kesho kujionea mwenyewe hiyo SUMU.