FROM NIGERIA "P-SQUARE SASA KUTUA BONGO NOVEMBER 23!

002.JP

004.JP
    Mtangazaji wa East Afrika Radio, Hillary Daudi (Zembwela)akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza ujio wa wasanii wa muziki wa kizazi kipya Peter na Paul Okoye maarufu kama  P – Square  kutoka nchini Nigeria pamoja na mdhamini Mkuu,Tarehe 23 Mwezi ujao ndipo watawasili nchini. Wasanii hao wataambatana na wasanii wengine 13 kutoka nchini humo. Pamoja nae katika Picha ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasilino wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa ambo ndio wadhamini wa onesho hilo.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt jijini Dar, Hillary Daudi wa East Afrika Radio, Amesema onesho hilo litakuwa la kipekee. P- Square wataongozana na wasanii wengine 13 ambao watatoa burudani ya Live Band siku hiyo Pamoja na wasanii wengine kutoka Tanzania.Wote tunatambua namna kundi hili linavyofanya vizuri ndani na nje ya bara la Afrika, licha ya kutoa burudani kwa mashabiki, pia litatoa fursa kwa wasanii wa ndani kujifunza kutoka kwa wasanii hawa vijana ambao wamepata mafanikio makubwa kutokana na kazi yao ya muziki,” alisema na kuongeza “hii itakuwa ni fursa ya kipekee kwa wasanii wetu wa bongo kujifunza kwa kuangalia wenzao wanavyofanya kazi”. Tutaendelea kuwaletea Habari zaidi za tour hiyo.