BIASHARA MATANGAZO !

Yaani Sio Mabango tu


Na Joseph Msami wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Matifa

Mfanyabiashara huyu mwenye asili ya Uhispania ambaye jina lake halikufahamika mara moja alinaswa katikati ya mji wa New York akiwa amevaa mabango yanayotangaza mavazi ya wanaume (suti) na kusambaza vipeperushi vinavyoelekeza wapi bidhaa hizo zinapatikana pamoja na mawasiliano.
Asili ya wakazi wa mji huu, kutingwa na shughuli na kutembea mwendo kasi muda mwingi kunawalazimu wafanyabiashara kubadili mbinu za kufikisha ujumbe wao ambapo badala ya kuongea na watu,wengi hutoa kadi za biashara zenye mawasiliano (business cards) au kuweka mabango yenye ujumbe husika.