SINGER-SHETTA KUZINDUA WIMBO WAKE MPYA "BONGE LA BWANA FT LINAH " TAREHE 25 NOV !!

                          
Bonge La Bwana ni wimbo wa Rapper Shetta uliotangazwa kutoka mwisho wa mwaka huu na kwasasa ipo tayari baada ya mabadiliko kufanyika. Awali Shetta alitangaza kufanya wimbo huu na komando Lady J Dee ila baada ya mabadiliko aliwekwa Linah . Shetta ameongea na DMK411 na kusema baada ya Lady J Dee kuskia beat na idea ya wimbo huu alimshauri afanye na msaani anaye endana nae kiumri zaidi ili ata akimwimbia Bonge la Bwana ieleweke zaidi, Fahamu kuwa Lady J Dee na Shetta bado watafanya wimbo mwingine ila sio huu. Baada ya kushauriwa hivyo Shetta aliona atakaye fanya vizuri kwenye Bonge la Bwana ni msanii Linah kutoka THT Na ndio amewekwa kwenye Wimbo huu kwa sasa. Kuhusu Video ,Tayari Adam wa Visual Lab anayo na anauskiliza kwahiyo muda wowote itaanza kufanyiwa kazi. Imesha thibitishwa kuwa Bonge La Bwana ni Shetta Ft Linah.

Kuhusu uzinduzi wa wimbo huu Shetta ameiambia DMK411 kuwa uzinduzi utafanyika maisha club Terehe 25 November na atasindikizwa na wasanii kama Jafarah ,Stereo, Shilole , Linah , Young Dee , Feruuz ,Suma Mnazareti na Pasha.