NWANKWO KANU ATEMBELEA WAGONJWA WA MOYO TAASISI YA JAKAYA KIKWETE HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI
Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria, Super Eagles, Nwankwo Kanu ambaye pia ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika akiwa katika Jengo la Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete lililopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako amewatembelea wagonjwa wa moyo jana. Kanu atakuwepo nchini kwa muda wa siku tano kushiriki shughuli mbalimbali za kampuni na kijamii.