TUZO ZA MTV MAMA KUFANYIKA LEO, DURBAN AFRIKA KUSINI


Msanii  wa Nigeria, David Adedeji Adeleke 'Davido' (kushoto) akiwa na Diamond Platnumz.
Mwigizaji maarufu nchini Marekani ambaye pia ni mchekeshaji, mwandishi wa muswada na mwongozaji wa filamu, Marlon Wayans anatarajiwa kuwa  msanii mkubwa atakayeongoza jukwaa katika hafla ya ugawaji wa Tuzo za MTV Africa Music Award 2014 zikatakazo tolewa leo jijini Durban Kwazulu - Natal nchini Afrika Kusini.
Hafla ya utoaji wa tuzo itafanyika katika Ukumbi wa Durbun International Convertion Center (ICC) katika mji wa Kwazulu-Natal, Afrika Kusini.

Tuzo hizo zinatarajiwa kurushwa live kuanzia saa tatu kamili usiku wa leo, kupitia MTV Base (Dstv Channel 322) na MTV ( Dstv Channel 130).

Katika tuzo hizo, Mwanamuziki wa Tanzania, Diamond anawania vipengele viwili ikiwemo Mwanamziki Bora wa Kiume akiwa na Anselmo Ralph ( wa Angola), Davido (Nigeria), Donald ( Afrika Kusini) na Wizkid (Nigeria).
Diamond pia anawania kipengele cha Kolabo Bora kupitia wimbo wa 'Number One' (Remix) (Tanzania/ Nigeria), wakiwa na Amani ft Radio na Weasel- 'Kiboko Changu' ( Kenya/ Uganda), Mafikizolo feat May D - 'Happiness' ( Afrika Kusini/ Nigeria), R2bees ft Wizkid - 'Slow Down' (Ghana/Nigeria) na Uhuru ft DJ Buckz, Oskido, Professor, Yuri Da Cunha - 'Y-tjukutja' (Afrika Kusini/Angola)
Tuzo anazowania Diamond
Wakati Watanzania wakishangilia ushindi wa Diamond katika tuzo za KTMA za hapa nyumbani, msanii huyu leo anawapa mtihani mgumu wengi kuamini kama ataweza kushinda tuzo hizo ili kufungua njia katika tuzo za kimataifa ikiwemo BET.Msimamizi mwingine wa Diamond ni meneja Mkubwa Fela ambae amethibitisha kwamba kwenye safari yake ya kuja South Africa ameambatana na Watanzania wengine saba ila kilichomfurahisha zaidi ni kwamba amekuja kukuta washkaji zake zaidi ya 20 wanaoishi Durban wameshanunua ticket tayari kwa ajili ya kumshangilia Diamond’
Watanzania waliofunga safari kutoka Tanzania mpaka Durban ni pamoja na Wema Sepetu, Aunt Ezekiel, Bab Tale, Salam ambae pia ni meneja wa Diamond, Mkubwa Fela, Watangazaji Sam Misago, B12, Adam Mchomvu, Millard Ayo, Shadee lakini pia Nancy Sumari na mpenzi wake Lucas, Ommy Dimpoz, Shetta na mpiga picha Michael Carter Mlingwa.