Gari la Chameleone lakamatwa Kwa kushindwa kulipa Kodi.


   Mwanamuziki Tajiri kuliko wote Afrika Mashariki Jose Chameleone amenyang'anywa Gari lake aina ya Cadilac Escalade baada ya Kushindwa kulipia Kodi yenye thamani ya jumla ya Shiling Milioni 7 za Uganda.
   Akizungumza kwa njia ya Simu na Swahili Meadia Group Chameleone alithibitisha kukamatwa kwa gari hilo akiwa anajiandaa na show yake kubwa ya Tubonge na akadai kuwa tatizo sio pesa bali nikwamba URA(Uganda Revenue Authority) walishindwa  Kuthibitisha ni vigezo gani walitumia kupata thamani ya kodi ya Shilingi Milioni 7.