OMMY DIMPOZ APAA LEO KUELEKEA TANZANIA NDANI YA BUSINESS CLASS YA EMIRATE !


OMMY DIMPOZ AKIWA NDANI YA EMIRATE BUSINESS CLASS AKIELEKEA TANZANIA
Mwanamuziki wa Bongo Flava aliyemaliza Tour yake ya kwanza nchini marekani Ommy Dimpoz ameondoka leo kuelekea Tanzania ambapo ana show inamsubiri kesho usiku
Dimpoz akiwa Na USA Tour Manager wake "DMK" wakiwa Airport huku akiwa amepozi na Kofia yake ya POZ KWA POZ "PKP" Kofia hizo zinapatikana kwa special orders only.
Kushoto ni Promoter na Tour Manager "DMK" Pamoja na (kulia)Mwanamuziki Mtanzania aishie Marekani "AJ UBAO" Wakiwa Airport Walipo Msindikiza Ommy Dimpoz(katikati)
Ommy Dimpoz amewashukuru Tanzania Wote kwa kumsupport na pia Kuwaambia miji ile ambayo hakupata nafasi ya kuitembelea kuwa wakae mkao wa kula kwani atarudi kwa part two mwezi december, Tour Yake hiyo Part two itakuwa katika miji ya New York, Dallas, Oakland Chicago na Boston, Pia aliwashukuru Mapromota wake kwa kumkatia Business Class ili aweze kupumzika vizuri akiwa safarini kwani ana Show Dar es salaam mara tu baada ya kutua anaenda moja kwa moja kwenye Show..BONGO FLAVA IKO JUU!