MZEE WA RUKSA-KUWA MGENI RASMI SHEREHE YA MIAKA MITATU YA VIJIMAMBO/TAMASHA LA UTAMADUNI WA KISWAHILI MAREKANI!!


Blog ya Vijimambo ikishirikiana na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini, Washington, DC, Marekani na Jumuiya ya Watanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia wanapanga kusheherekea miaka 3 ya Vijimambo na kukuletea tamasha ni kuendeleza lugha na utamaduni wa Kiswahili hapa Marekani ili watoto wanaoishi huku waweze kuendeleza matumizi ya lugha hii na utamaduni wake kizazi hadi kizazi. 

Siku ya July 6, 2013  hapa DMV kwenye Hall la Hampton Conference Center lililopo 
207 w Hampton Pl, 
Capitol Height, MD

Mambo mengi yatakuwepo, Vikundi mbalimbali vya utamaduni, Asya Idarous mwanamitindo ya mavazi kutoka Tanzania akishirikiana na hapa Marekani, vyakula vya Kitanzania, Wasanii kutoka nyumbani na hapa Marekani yote ni kudumisha utamaduni wetu wa kiswahili

TEGA SIKIO, HABARI ZAIDI ZITAFUATA
-------------------------------------------------------
kwa wajasiliamali ambao wangepenga kudhamini na kuijipatia meza ya kutangaza bidhaa au shughuli wazifanyazo tafadhali wasiliana 301 613 5165, 301 661 6696 na 301 792 8562 mwisho ni June 15, 2013 Asante
HABARI HII KWA HISANI YA VIJIMAMBO BLOG!!