RUGE MTAHABA KASHINDWA KUJIBU SHUTUMA NA HOJA ZA JIDE


                          
Boss wa Clouds FM  Bw.Ruge Mutahaba katika mahamuzi ya "hasira za mkizi"

  Ruge Mutahaba kashindwa kujibu shutuma za comando Lady Jay Dee

  Wasanii hamkeni kujua nani mchawi wa kazi zenu

Watanzania leo tulikua tukimsikiliza mkurugenzi wa utafiti wa redio Clouds FM Bw.Ruge Mtahaba katika mahojiano
na redio yake ya clouds fm mahojiano ambayo tulikua tukitegemea boss Ruge ajibu shutuma dhidi yake za kumtilia kauzibe katika kupata ridhiki mwanamuziki Lady Jay Dee bint machozi, katika mahojiano hayo ambayo sisi wasikilizaji tunayafananisha sawa na KESI YA NYANI mwamuzi awe Ngedere .
Tulichokua tunakitegemea katika mahojiano ni majibu ya shutuma dhidi ya Bw.Ruge lakini cha kushangaza Ruge kashindwa kabisa kujibu shutuma zinazomkabiri baadala yake akawa anarusha rushua maneno na kuhusisha mifano ya 
wasanii walishuka na nani kapanda , na kuenda nje ya hoja ya msingi,mwisho wa mahojiano Bw.Ruge alikurupuka kwa
kauli za kuamrisha kuwa ni maarufu kupiga nyimbo za kizazi kipya (Bongo Fleva) kwa mda wa siku nzima katika kituo cha clouds fm.

Sasa watanzania tunajiuliza hivi redio ya Clouds FM au Redio ya Ruge na wasanii pamoja na sisi wanachi nani ? muhimu.
kwa karne hii ambayo taifa lina vituo vya redio zaidi ya 80?
Kwani wasanii wanamuhitaji sana Ruge na mshirika wake Bw.Kusaga,yaani wao ndio tuseme miungu ya wasanii?
Wananchi walio wengi wanamuunga mkono Lady Jay Dee kwa kutokukubali afanywe ngazi au kitendea kazi cha kuwanufaisha wanyonyaji katika soko la muziki,na kahamua kujitegemea.mahamuzi hayo ya Jay Dee ndio yanamfanya Jide atake kugeuzwa   "Kondoo wa Sadaka"  .

 MRADI WA RUGE MTAHABA KATIKA SEKTA HII YA MUZIKI NI KUUA MUZIKI WA DANSI NA TAARABU NA KUJENGA MSINGI WA UTAMADUNI NA MZIKI WA KIZAZI KIPYA .

Ukisikiliza sana maelezo ya Ruge katika mahojiano utagundua wazi kuwa alijenga au alijaribu kujenga mtandao wa
kuwamiliki na kuwajenga wanamuziki wa kizazi kipya kwa manufaa yake,yaani mwanamuziki hasipoingizwa katika
mtandao huu basi hatojulikana na kazi zake azitotambulika ,yaani mtandao ambao pia unampendekeza msanii gani
aukubalike kupewa tuzo hata kama si msanii mzuri, mtandao huu pia unatumika kama sululu la kuuchimbia kaburi
muziki wa dansi na muziki wa taarabu,mtandao huu pia unawalazimisha watanzania walio wengi muziki gani wa 
kusikiliza, na mara nyingine kuwalazimisha wanamuziki nini cha kupiga( Beat) n.k.

Leo Ruge anapomsema Lady Jay Dee ampe kijiti mwingine na Lady Jay Dee anaposema yeye ni Lady Jay dee
anapiga muziki kwa maisha yake na kuwalidhisha washabiki wake,hakuna haja ya kupokezana vijiti katika gemu
la muziki. Bali mfumo huu kupokezana vijiti ni mfumo unaoitwa "Ruge Mtahaba  System" na wasananii wamesha
istukia kuwa si mfumo mzuri. Je ? wanamuziki wapo tayari kufanywa kete za kuchezea bao au chess!
kwanini? lazima wasanii wapate pumzi ya uhai kutoka katika mtandao wa Ruge? hivi wasanii hawezi kusimama
kidete na kuungana kwa pamoja wakajipigania na kukataa kufanywa wapagazi katika sekta hii? Ruge kaonyesha
Kiburi kwa kusema mziki wa bongo flava usipigwe kwa siku nzima redioni Clouds ! Sasa wasanii na nyinyi
Onyesheni mshikamano na msimamo wenu kwa Ruge,kuwa nanyi ni muhimu kwa jamii ya watanzania.

Je ? Nani mchawi wa kazi za wasanii na muziki wa Tanzania?

Watanzania na serikali ya Tanzania imeshuhudia kuangushwa kwa makusudi muziki wa dansi wa tanzania,
na kuchimbiwa kaburi utamaduni na sanaa za maonyesho wa watanzania,ujuma ambazo zinafanywa na mtandao
ya siri ya wajanja wanaujumu utamaduni na muziki wa watanzania.
Na wanamtandao ambao wanaangaliwa macho bila ya kufanywa chochote na watanzania au kuchukuliwa hatua zozote
na serikali kupitia  idara husika.
Leo watanzania tunajiuliza hivi hawa akina Ruge Mtahaba wanazijua historia ya muziki wa Tanzania? na misingi ya
Miziki wa Tanzania, na wale waliojitoa waenga muhanga katika kujenga misingi hiyo imara? mbona nchi za wenzetu
wanaendeleza misingi na miziki yao ya awali,kama ilivyo taarabu na muziki wa dansi.
Inakuaje leo hapa kuna baadhi ya wajanja wasiojua hata historia ya muziki wa tanzania wanatuchagulia nini? cha kusikiliza na kutufanya watanzania kuwa guo guo wa kufuata
utamaduni mpya wanaoubuni wajanja.
 "JOTO HASIRA"  KUNA HAJA YA KUWAFUKUZA KAZI NA KUVUNJA MTANDAO HUU UNAUJUMU
  UTAMADUNI ,MUZIKI NA WASANII WATANZANIA