MCHEZA FILAMU WA BONGO-JB KUJITOSA KUGOMBEA UBENGE MWAKA 2015 !


MWIGIZAJI ‘namba wani’ Bongo mwenye heshima kubwa, Jacob Stephen Mbura ‘JB’ yupo mguu sawa kuingia kwenye ulingo wa siasa kwa kugombea ubunge mwaka 2015.
Akizungumza na paparazi wetu jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, JB alisema ameamua kuweka wazi ndoto yake hiyo ya miaka mingi ambapo ilikuwa kuitumikia jamii ya Kitanzania.
“Nimeamua kuweka wazi kwamba mwaka 2015 nitajitosa rasmi kwenye kinyang’anyiro cha ubunge. Nia ninayo, uwezo ninao na sababu pia ninayo,…