MCHEZAJI WA SIMBA OKWI-AUZWA KWA SH MIL 450 !!


Emmanuel-Okwi580
Klabu ya Simba imemuuza aliyekuwa mchezaji wake na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uganda, Uganda Cranes Emmanuel Okwi kwa klabu ya nchini Tunisia ya Etoile Sportive kwa dau la dola 300,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 450 za Tanzania.
Okwi alijiunga na Simba SC mwaka 2010 kutoka SC Villa kwa ada ya dola 40,000.
Baada ya kukamilisha mkataba wa awali December mwaka jana, Okwi aliongeza mkataba wa miaka miwili na Simba SC ambayo kabla hajaanza kuitumikia shavu la Sahel likaibuka.
Katika ukurasa wake wa Facebook aliandika kuonesha furaha yake kwa kusema, “Oh God I thank U for making me reach this far in Life for without U I wouldn’t be where I am today.”
Aliongeza; “Am officially a player of Etoile Sportive Du Sahel, it’s really a new challenge and a big step for me in my career.. Let me take this chance to thank all Simba fans and officials for the support you gave me.. U were really special to me, god bless u all.. Alluta continua.