PESA ZILIZOPATIKA KWENYE SHOW YA P SQUARE UGANDA ZIMEIBIWA...MAPROMOTER WAZIMIA NA KULAZWA!


Waandaji wa show ya hivi karibuni ya P-Square nchini Uganda iliyopewa jina la Chop Ma Money Concert wanaugulia maumivu baada ya kiasi kikubwa che fedha kilichopatikana kwenye show hiyo kupotea. Zaidi ya shilingi milioni 450 za Uganda zilizokuwa zimekusanywa kutoka kwenye vituo mbali mbali vya kuuzia tiketi zimepotea.
Pesa zilizokusanywa getini nazo ziliibiwa na hivyo kumfanya mkurugenzi wa Silverback Investments, Yvonne miongoni mwa waandaji wa show hiyo alizimia baada ya kugundua kuwa hela hizo zimepotea.
Polisi wanasema washukiwa wa wizi wa fedha hizo wamekimbilia DRC. Ama kweli..kazi ipo.....Mapromoter tunakazi sanaaaaaaaaaaaaaa...Africa noma !