MIAKA 7 YA TANZANIA HOUSE OF TALENT (THT) YAFUNIKA DAR LIVE !Familia ya THT ikiwa jukwaani wakati wa kusherehekea miaka 7 toka kuanzishwa.
Linah akiwa stejini (  Msanii toka THT).
Shilole na kundi lake wakilishambulia jukwaa la Dar Live.
Vijana wa THT wakiwasha moto wakati wa sherehe yao ya kutimiza miaka 7 ndani ya Dar Live usiku wa kuamkia leo.
Msanii Ben Pol akiwajibika stejini.
Shetta akiwapa raha mashabiki.
Dogo Aslay akiwadatisha mashabiki.
Ommy Dimpoz akiimba na mashabiki waliofurika ndani ya Dar Live.
Mwanadada Sundi Gaga kutoka THT akionyesha swagga zake jukwaani.
Rachel akiwapagawisha mashabiki wake(msanii toka THT)
Juma Mataluma akifanya mambo(toka THT)
...Mpaka chini.
Shangwe zikizidi kukolea ndani ya Dar Live.
Ben Pol akicheza na mashabiki wake.
Msanii Ditto akiwapa tano mashabiki (toka THT)
WASANII wa nyumba ya vipaji, Tanzania House of Tallent ‘THT’ usiku wa kuamkia leo waliangusha bonge la pati ndani ya Ukumbi wa Dar live uliopo Mabagala jijini Dar kusherehekea miaka 7 ya kuanzishwa kundi hilo la kukuza vipaji. Katika pati hiyo wasanii mbalimbali wa muziki walitoa burudani hasa wasanii wenyewe wa THT. Pichani juu ni baadhi ya matukio yaliyojili ukumbini hapo.
(PICHA NA MUSSA MATEJA)