MWANAMITINDO-MUSTAFA HASSANALI " KUSHIRIKI ARISE MAGAZINE FASHION SHOW..KULE NIGERIA

Mbunifu wa mitindo maarufu kutoka nchini Tanzania,Mustafa Hassanali, ni miongoni wabunifu wa mitindo 77 kutoka mabara 6 ya ulimwengu wanaotarajiwa kushiriki katika maonyesho ya mavazi yajulikanayo kama  ARISE Magazine Fashion Week(AMFW) yanayotarajiwa kufanyikia jijini Lagos nchini Nigeria mwezi ujao.
Maonyesho ya mwaka huu  yatafanyikia katika viwanja vya hoteli maarufu na ya kifahari ya Federal Palace Hotel ya jijini Lagos yataanza Siku ya Jumanne tarehe 6 Machi na kumalizika Jumapili ya tarehe 11 Machi (Tuesday 6th March-Sunday 11th March). Haya yanafuatia yale ya mwaka jana ambayo yalishuhudiwa na zaidi ya wageni 5,000 wakitazama ubunifu kutoka kwa wabunifu 51 uliowekwa jukwaani na wanamitindo 81.
Mustafa Hassanali ni mbunifu wa mitindo pekee kutoka nchini Tanzania anayetarajiwa kushiriki katika maonyesho hayo ambayo yanazidi kujipatia umaarufu.Orodha kamili ya wabunifu wa mitindo wanaotarajiwa kushiriki katika maonyesho hayo ni;
Adama-Paris (Senegal/France), Amine Bendriouich Couture and BS (Germany/Morocco), Amrapali (India), Angelo Van Mol (Belgium/Ghana), Be-Grey (Nigeria), Bestow Elan (UK/Ghana), Bridget Awosika (Nigeria), Buki Akib (UK/Nigeria), CHICHIA (UK/Tanzania), Christie Brown (Ghana), CLAN (Nigeria), David David London (UK), Davida (Nigeria), Duaba Serwa (Ghana), Ejiro Amos Tafiri(Nigeria), Eki Orleans (UK/Nigeria), Frank Osodi (Nigeria), Funlayo Déri (UK/Nigeria), Gavin Rajah (South Africa), Gloria Wavamuno (Uganda), HOUSE of DIVAS (Nigeria), House of Farrah (Nigeria), House of Nwocha (Nigeria), ICONIC INVANITY (Nigeria), Imane Ayissi (France/Cameroon), Jacob Kimmie (UK/South Africa), Jewel by Lisa (Nigeria), Kastle Designs & Treasure Chest (USA/Ghana), Kaveke (Kenya/UK), Kevan Hall (USA), Kezia Frederick (UK/St.Lucia), Kiki Clothing (Ghana), Kinabuti (Italy), Klûk-CGDT (South Africa), Koke (Botswana/India), Korto Momolu (USA/Liberia), Lanre Da Silva Ajayi (Nigeria), LaQuan Smith (USA), Laurenceairline (France/Ivory Coast), Loza Maléomsho (USA/Ivory Coast), Madam Wokie’s Couture (Sierra Leone), Mai Atafo(Nigeria), Maki-Oh (Nigeria), Mataano (USA/Somalia), Meena (Nigeria), Mustafa Hassanali (Tanzania), NKWO (UK/Nigeria), Odio Mimonet (Nigeria), Okunoren Twins (Nigeria), Osman (UK), Paul Hervé ELISABETH (Martinique), Poisa (Kenya), Re Bahia (UK/Nigeria), Sandra Kennedy (Jamaica), Sandra Muendane (Mozambique/Portugal), Sunny Rose (Nigeria/UK), Taibo Bacar (Mozambique),the Vessel. By Lois (USA/Jamaica), Tiffany Amber (Nigeria), Timo Welland (USA/South Africa), Tsemaye Binitie (UK/Nigeria), U.Mi-1 (UK/Nigeria), Virgos Lounge (UK/Nigeria), Viv La Resistance (Nigeria), William Okpo (USA/Nigeria) and Zekaryas Solomon (Eritrea/UK).
BC inapenda kumpongeza Mustafa Hassanali kwa mafanikio haya na juhudi zake katika kuitangaza Tanzania kupitia mitindo na ubunifu.