MSANII KUTOKA TANZANIA "DIAMOND" AHUKUMIWA KWENDA JELA MIEZI 6 AU FAINI SH 50.000

MSANII nyota wa muziki wa Kizazi kipya Diamond na wenzake wamekubali kosa la kumshambulia mmiliki wa mtandao huu Bw.Francis Godwin na kuhukumiwa kwenda jela MIEZI 6 Kila mmoja ama kulipa faini shilingi 50,000 kwa Kila mmoja ikiwa ni Pamoja na kulipa sh. 30,000 kwa Godwin kila mmoja,Lakini inasemekana mwandishi kakataa hela hizo na atafungua kesi ya madai ili halipwe thamani ya Vyombo vyake vya kazi vilivyo haribiwa na msanii huyo na wenzake