ALI KIBA NA NEYO...USO KWA USO


King Kiba kutoka Tanzania, anaye nyimbo kama “Mwana” na “Chekecha Cheketua” akutana na mwanamuziki kutoka amerikani: NE-YO, anayefahamika kama mwanamuziki na mwandikaji wa muziki bora kama “Let me love you,” “Sexy Love” and “She Knows”. 

Hao wawili walikutana Nairobi katika Coke Studio Africa. Alikiba ni baadhi ya wanamuziki watano: Wangechi (Kenya), Dama Do Bling (Mozambique), Ice Prince (Nigeria) na Maurice Kirya (Uganda) pamoja na Alikiba. Wawili hao, pamoja na wenzao, walizugumzia muziki wa Afrika na pia kurecord nyimbo mpya.

King Kiba yuko Nairobi na anatarajiwa kufanya wimbo na hao wanamuziki katika format mpya ya Coke Studio Africa season 3, itakayozinduliwa mnamo Oktoba mwaka huu. Alikiba yuko Coke Studio Africa kwa mara ya kwanza msimu huu. Ashashirikiana na Victoria Kimani (Kenya na Tanzania) katika nyimbo za mash-up.