DIAMOND ASHINDA TUZO YA BEST AFRICAN ENTERTAINER ..NIYA 14 NDANI YA MWAKA 2014 PEKEE

Promoter  " DMK " Baada ya kuipokea Tuzo Hiyo ya IRAWMA kwa niaba ya Diamond .Diamond hakuweza kufika kwenye tuzo hizo zilizofanyikia Florida kwa mwaka huu kutokana na tarehe kugongana na shughuli zake za kazi.Diamond ameweza kujishindia tuzo 14 mwaka huu pekee ikiwa ni pamoja na Tuzo 7 za Kilimanjaro Award na 7 za kimataifa.Bwana "DMK" amepokea Tuzo hiyo  kwa niaba ya Msanii Diamond na kwasasa Tuzo hiyo iko Njiani Kuelekea Tanzania.Mungu azidi kumjalia afya Njema Mwanamuziki huyo kwani anaipeperusha Vyema Bendera ya Tanzania.