NAY AVUNJA NDOA YA SKAINA WA BONGO MOVIE



Nay wa Mitego 
Skaina
SASA hakuna ubishi kuwa, ile ndoa iliyofungwa kwa mbwembwe na kuvunjika kabla ya mwezi mmoja kati ya msanii wa filamu za Kibongo, Skyner Ally ‘Skaina’ na Saad Omar, chanzo ni Mwanabongo Fleva, Emmanuel Eribaliki ‘Nay wa Mitego’. 
Habari za awali zilisema kuwa, ndoa ya Skaina iliingia mdudu baada ya mumewe kugundua kuwa alinunua ‘mbuzi kwenye gunia’, kwani bidada huyo alikuwa na ujauzito wa mtu mwingine.
Hata hivyo, minong’ono ilikuwa inasema kuwa, mimba hiyo ilikuwa ya Nay ingawa awali, hakuna aliyekuwa tayari kufafanua kuhusiana na ishu hiyo. 




Ndoa ya wawili hao ilifungwa Oktoba 7, 2011 nyumbani kwa dada yake, Magomeni – Mapipa, Dar na kufika tamati kabla ya mwezi Novemba, dah!

Ripoti zilizopo kwenye makabrasha ya Risasi Mchanganyiko zinaonesha kuwa, baada ya Skaina kutemwa na Saad alimweleza Nay sababu na kutimkia kwao Iringa ambapo alipojifungua alimweleza ukweli mwenzi wake huyo kuhusu ujio wa mtoto wao.


.
 Wawili hao wameelezwa kuwa na mawasiliano ya karibu lakini ya siri kwa muda mrefu ila hivi karibuni, wote waliamua kuutua mzigo huo na kuweka mambo hadharani ambapo kwa upande wa Skaina alisema: “Nadhani mmechelewa tu kujua, lakini habari ndiyo hiyo.”
Nay alipoulizwa, alijibu kwa kifupi sana: “Ni kweli lakini ni mambo ambayo huwa sipendi kuyazungumzia sana.”
 Ili kuthibitisha ukweli huo, wikiendi iliyopita, baada ya Nay kutwaa tuzo moja ya Kili katika kipengele cha Wimbo Bora wa Kushirikiana, Skaina alitupia maneno ya kumpongeza Nay katika ukurasa wake kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram yaliyosema: “Hongera baba mtoto wangu kwa kuchukua tuzo, Mungu akuzidishie baraka na maisha marefu ili mwakani uweze kuchukua tuzo nyingi zaidi. Navutiwa sana na kazi zako dady wetu (akimaanisha yeye na mwanaye).”