MSIBA DMV NA TANZANIA !

Familia ya Bw na Bibi Keith Thornton wa Capital Heights Md wanasikitika kutangaza kifo cha baba mzazi wa Beatrice Kilima. Mzee Kilima , aliyefariki dunia Jumanne Oktoba 22 jijini Dar es salaam Tanzania. Baada ya kuugua kwa muda mrefu. Kama desturi yetu tumpe pole mwenzetu lakini kwa hivi sasa Beatrice yuko njiani kuelekea Tanzania kwa ajili ya mazishi lakini tumkumbuke kwenye sala zetu na akirudi tutawajulisha. Asanteni