Baada ya Ruge Mutahaba kuzungumza asubuhi ya leo kuhusu kinachoendelea kati yao na mwanamuziki Lady Jay Dee kwenye mitandao tofauti ya kijamii, mwanadada huyo Komando ambaye kwa sasa antamba kwa jina la Anaconda amefunguka tena kupitia ukurasa wake wa facebook na kuandika kifuatacho:
"Kama mtakumbuka niliahidi kutoa awamu ya pili tar 15 au 17 May na ahadi ni deni. Japo naona mbali ila nitafanya hivyo, bado nina mengi sana ya kuzungumza kuhusu Ruge na wenzake... Ile ilikuwa ni trailer tu, Movie ndio linaanza sasa #TeamAnaconda no surrender".
|
Soma hapa chini alicho kisema Ruge Leo ndani ya Power Breakfast
Haya ni mazungumzo ya Ruge Mutahaba na msimamo wa Clouds juu ya mwanamuziki Lady Jay Dee, mazungumzo ambayo yalifanyika kupitia kipindi cha Clouds fm cha cha Power Breakfast , mbali na mengi aliyoyaongea haya ni machache kti ya mengi na hivi ndivyo alianza:
RUGE:
As a country we need to discuss issue kwa maendeleo ya nchi, tuachane na ku-discuss ishu hizi kama personal issue.
Ni kweli kwamba tulikuwa hatutaki kulizungumzia hili na hata sasa, ila kutokana na msukumo ladba ni vizuri kuliongelea, ila uamuzi ulikuwa ni wetu kama tuongee au tusiongee.
Sometimes unahisi unahitaji kusikia upande wa pili, kwa binadamu yoyote, kwa maana kuna watu ambao wanaishi mbali na hapa mjini kama Kigoma nao wanapenda kujua juu ya swala hili kwa upande wa pili likoje.
Ila tu niseme ni tatizo la mtu binafsi halina sababu ya kujadiliwa na kufanywa kama ni suala la kitaifa, sababu sura inayowekwa ni kama kitu kikubwa sana, binafsi bado sijajua nini hasa tatizo la kinachojadiliwa.
Ikumbukwe kwamba Clouds ni chombo binafsi, ni chombo ambacho kilianzishwa kwa kufata sheria zote, na sisi tulichagua namna sisi tukavyoendesha redio yetu.
Kama biashara yoyote na sisi tunafanya biashara kutokana na mipango yetu, na ndio maana kwa kipindi cha miaka 10 tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Hakua anayefanya sawa duniani akakosa kulaumiwa, sisi ni binadamu na tuna makosa ya kibinadamu kama binadamu wa kawaida.
Nakumbuka ilikuwa ni tarehe 14-12 siku ambayo Lady Jay Dee kwa mara ya kwanza alipoandika kwenye mitandao ya kijamii ujumbe uliosema “ukinikosea nitakusimamisha na sitokuamsha tena”,
Niliambiwa na jamaa wa Bongo5 na nikaamua kumpigia simu JD siku hiyo na nikamwambia kwamba, kuna maneno nimeambiwa kwamba wewe umeandika, yeye akasema hapana, namini nikamwambia sikiliza nikwambie kwa ninavyokwambia wewe , haya mambo hayafai.
Baada ya kukata simu dk 10 akanitumia sms mfululizo, ya kwanza aliandika “Nililipa matangazo yangu ya laki 2 na 70, nimeambiwa kwamba umekataza yasipigwe.
Sms nyingine ilisema “unaruhusu watangazaji wako wanitukane na kui-promote bendi yako ya Skylite”.
Huku akiendelea Ruge akasema, unajua kwamba sisi biashara yetu ni matangazo, kwa nini nikatae, mbona siku zote tunayarusha matangazo yao? Na Gadna kila siku anakuwepo hapa kufanya matangazo? Ni swala la yeye kupita tu chini ni kuuliza kama kweli matangazo hayarushwi.
Na kitu kingine ni kwamba, sio kweli na siwezi kumruhusu mtangazaji yeyote amtukane redioni.
Mimi ishu ya skylite, Skylite wanalipa matangazo kama wateja na bendi nyingine zinavyolipia, na huwa tunawapa bonsai kama ambavyo huwa tunampa yeye JD.
Nilimwambia JD angalia maana ni kweli kwamba Skylite wanakuja juu aangalie, hakika kuna upotoshwaji Skylite kuhusishwa Clouds, Skylite ni ya Sebastian Ndege, yeye analipa matangazo kama wengine wanavyolipa, akilipa laki 2 tunampa matangazo ya laki mbili kama bonasi.
Skylite ilichukua wanamuziki watatu wa Machozi Bendi, kama ambavyo ilifanya kwa bendi Banana na TID. Kiukweli wakati haya yanaendelea mimi nilikuwa safari niliporudi baada ya hiyo tarehe 14, nikaona mbona hakuna jambo la kuzungumza au kujadili, katika yote ni nini anacholalamika hasa? Mbona sioni tatizo?
Ishu ya kusema kwamba nyimbo zake hazipigwi, unajua hapa kwetu kuna systeme ambayo inaweza kuangalia na kujua wimbo katika muda flani ulichezwa mara ngapi, kupitia systeme hiyo tuliangalia na kuona kwamba wimbo wake wa Joto Hasira ulichezwa mara 46 mpaka siku tunasema hatupigi nyimbo zake.
Tarehe 12-02 niliongea na Gadna na sio Jd juu ya kwenda kuazima stuli kwa ajili ya shooting, na tukazitumia na kisha tulizirudisha.
Ni kweli kwamba tulikaa kikao binafsi sikuona kama kuna haja ya kutopiga nyimbo za JD, baada ya kutuma sms ya kwamba sisi tunaogopa ndipo tukasema Redio ina policy kwa utaratibu wetu, kwa anayetutukana, kutukebehi au maneno yoyot, basi nasi tutatumia njia zetu, na mpaka mtu huyo aje kwetu na tuongee na ku-apologize.
Mbona Diamond nyimbo zake hazipigwi Magic fm mwezi wa saba sasa, kuna kipindi Fulani East Afrika walikuwa hawazipigi nyimbo za Ray C na pia za Alikiba.
Sikuwahi kuona kwa nini jambo hilo kufanywa la kitaifa.
Kuna Redio 82 hapa nchini, na mtu anapokwambia achane kupiga nyimbo yangu, kwa maana asipotaka yeye mwenye kwa kauli yake tusipige nyimbo yake, basi tunacha.
Ni utaratibu tu….
Sioni tatizo la wananchi kulifanya jambo hili kama la kitaifa, kuna fulsa ya kujadili mambo mengi, kama ingekuwa mtu wa kugalagala chini kwa kuchukuliwa wanamuziki basi angekuwa ni Asha Baraka, ila ila kila siku kwa zaidi ya miaka 10 sasa anaamka anasimama, ndivyo ambavyo Lady Jay Dee anapaswa kufanya.
Historia ya JD ni ndefu, kwa mara ya kwanza nilimsikiliza kwenye Redio yetu kupitia kipindi cha Taji liundi cha Apex, alikwa studio anarap, nikamwambia Taji nahitaji kesho aje ofisini, nilipoongea nae nikampa kazi ya kutangaza, alikaa kwa kipindi cha mwaka mzima bila kuimba, mara ya kwanza kumuweke ilikuwa ni kwenye wimbo wa Baba wa Taifa mwaka 99.
Nikasema huyu mtu ni msanii mzuri na aanze kuimba, tulirekodi kwa Mika Mwamba na kwa msaada wa Mzee Muta.
Sisi tukanzisha project ya Smooth Vibe yenye lengo la kuwajenga wasanii, kisha tukawambia mziki ni full time job na tuliwauliza je mnachagua kuimba au utangazaji? Lady Jd na Ray C wakachagua kuimba na Fina akaamua kuendelea na utangazaji.
Ilipofika miaka mitano na tulipoona project imekwenda vizu tukaseama tuiache , tukaachana na project hiyo na yeye aaendelea zake.
Kinachotuhuzunisha ni kwamba yeye ni kioo cha wasanii wachanga ambao wanatakiwa kuiga mfano wake kwa yale mazuri, na hapa ndipo penye taizo ambalo ni kuachiana kijiti, tatizo ambalo ni kubwa kwa wanamuziki wengi kujiandaa.
JD anatakiwa ajitahidi kutengeneza uwazi kwa watu wajaribu kuelewa, sisi ni watu kama yeye, anashindwa basi atafute watu, na kama kuna tatizo la kitaasisi, mimi nipo wazi tayari kukutanana naye na kutafuta muafaka juu ya hili.
Mtu kama Lady Jay Dee anapaswa kufikisha malalamiko yake kwa sehemu husika huku akiwa na vielelezo ili tuone muafaka wake. Ni vyema kuwaandaa wasanii wetu na wao wajiandae, naamini bado mda upo kwake yeye, cha msingi ni kwa yeye kurudi na kulisoma soko.
Swala la Clouds kwamba inataka kuuwa muziki wa bongo fleva kwa makusudi, Clouds inategemea muziki wa bongo fleva kama mahudhui ya kipindi. Clouds kila weekend ndio Redio peke yake inayotoa udhamini kwa wasanii kufanya show zao Maisha na Bilicanas. Tamasha letu tunalofanya pekee ni Fiesta ndani ya miezi miwili kwa mwaka, hii ina maana kwa miezi mingine 10 wasanii huwa wanafanya show zao zaidi yah ii ya kwetu.
Swala kwamba tulitaka kumpa laki nane akakataa, ni swalala makubaliano, ni kama vile mbavyo unweza kumpa msanii million mbili akakataa au mwengine ukampa laki sita akakubali, ni swala la makubaliano tu na ndivyo biashara hii na nyingineyo kwa vile ilivyo. Ni kama yeye aliposhindwana Linah na Barnaba sababu ya kiwango cha hela ambacho alitaka kuwapa.
Mimi nafikiri, JD inabidi akaze buti, anapigana wrong war, Skylite inamsumbua na akubaliane na ukweli kwamba hilo ndilo tatizo lake. Sielewi connection ya Nyumbani Lounge kwa Clouds na Ruge, binafsi nintachojua vita zake azielekeze kwa Skylite Bend na inabidi azielekeze huko, na aangalie tatizo lilitotokea Nyumbani Lounge naamini hiyo ndiyo sababu kuu.
Cha msingi atafute mtu mwenye busara aangalie hili jambo hili litaishaje.
Kwa kumalizia, hii nchi sasa na vyombo vinavyohusika inabidi virudi na kufanya kazi zake ipasavyo kwa mambo mbalimbali yanayotokea kwenye mitandao.
Swala la kulaumiana halitatukuza, sisi ni Redio binafsi na tutafanya kile tunachotakiwa kufanya kwa matakwa ya walio wengi, chochote kinachotokea katikati.
Hii ni redio binafsi na sisi tuna taratibu zetu, kama ambavyo tuliwa kupiga nyimbo za wanawake kwa siku nzima basi na kuanzia sasa leo tusipige bongo fleva.
Msimamo wa kampuni, hili jambo hili hatutalizungumza, ila tunamtakia kila la heri kwenye show yake ya tarehe 31, ila atakapokuwa tayari kuendelea kufanya biashara na saisi katika zile redio 82 tutakuwa tayari kufanya kazi naye.