MOHAMED MATOPE AELEZEA KUHUSU KENYA-TIRIRIKA !


KWANINI KOTI YA KIMATAIFA (ICC) IMECHEMSHA KWENYE UCHAGUZI WA KENYA?
                                 BY MOHAMED MATOPE

Wakenya wengi walikuwa hawaijui International criminal court ( ICC), Koti ya Kimataifa mpaka wakati Raisi Uhuru Kenyatta na Makamu wake William Ruto waliposhitakiwa. Vile vile wafrika  wengi wanaelewa  kwamba  watu wanaoshitakiwa kwenye koti ya kimataifa ni viongozi wa nchi wanaotawala kwa mabavu na wauwaji wa raia wowote wanaowapinga kisiasa kama, Charles Taylor wa Liberia au viongozi wa vita vya misituni vya kuipinga serikali tawala (Warlords)  kama Joseph Kony wa Uganda .

ICC ni koti ya kimataifa iliundwa mwaka 2003, koti hii ina mamlaka ya kuwahukumu watuhumiwa wa makosa ya mauwaji ya kipimo cha juu (genocide), crimes against humanity na war crimes ndani ya Mtaifa yote yaliyosaini chata ya Koti ya Kimataifa.

Cha kustaabisha ni kwamba, Raisi Kenyatta anashutumiwa na ICC kwa kosa la crime agaist humanity,  kwa kushiriki kwake kwenye mauwaji ya Wakenya baada ya uchaguzi wa Raisi wa Kenya wa mwaka 2007. Mashitaka ya Kenyatta kwenye koti ya kimataifa ni sawa na mashitaka yanayomkabiri Joseph Kony  wa Lord’s Resistance Army(LRA) ya Uganda  na  Bosco Ntaganda kamanda Patriotic Force for the Liberation of the Congo (FPLC).

Wakenya wengi wanaomjua Kenyatta, hawajawahi kumuona amevaa nguo za jeshi, au ameshika bunduki, au yuko msituni akiwa amezungukwa na vijana wadogo  wenye AK47 machine gun. Wakenya wanamjua Kenyatta kama Mtoto wa baba wa taifa Jomo Kenyatta ,mfanyabiashara , mwanasiasa,mkikuyu na mtu anayeipenda Nchi yake.

Mauwaji ya Kenya ya mwaka 2007-2008, yalitokea baada ya uchaguzi wa Raisi wa mwaka 2007, mauwaji hayo yalisababiswa na vita kati ya makabila ya Wajaruo na Wakikuyu, pamoja na Wakikuyu na Wakalinjin.Vita hivi vilianza baada ya  mgombea uraisi   Raila Odinga (mjaruo) alipokataa kukubaliana na matokeo yaliyotangazwa na Tume ya uchaguzi ya Kenya, ambayo ilimtangaza  Raisi Mwai Kibaki (Mkikuyu) kuwa mshindi wa kura za Uraisi.  

Ukweli wa mambo ni hivi, Kenyatta na Ruto hawakuwa wagombea wa uraisi kwenye uchaguzi wa mwaka 2007.  Swali linakuja, kama Kenyatta na Ruto hawakugombea uraisi,  kwanini wameshitakiwa  kama waanzilishi wa vurugu zilizofuata baada ya uchaguzi huo?

Vile vile watu wanajiuliza, kwanini kesi ya Kenyatta na Ruto ilipelelezwa kwa kasi kubwa, na mashitaka yakaletwa  mbele ya jaji wa mahakama ya kimataifa miezi saba kabla ya uchaguzi mkuu? Kama ICC inaweza kuendesha kesi kwa kasi hivyo, mbona haijamshitaki mtu yeyote kwa crime against humanity  kuhusiana na vita vya Iraq  na afganistani,ambapo maelfu ya raia wameuwawa  na vita vimekuwa vinaendelea zaidi ya miaka kumi sasa?  

Vilevile watu wanajiuliza hivi sasa imeshapita miaka miwili tangu vita vya Syria vianze na ICC bado inapeleleza tuhuma za war crimes katika mgogoro wa nchi hiyo, kwanini inachukuwa muda mrefu kuwaleta watuhumiwa kizimbani? ICC ipo wapi kwenye vita vya Israel na Palestina? Au Migogo ya  Ulaya ya Mashariki?

Pamoja na hayo vile vile  watu wengi  wanahituhumu  koti ya kimataifa kuwa ni  fimbo ambayo Mataifa ya Magharibi wanaitumia kuwachapa viongozi wa  Afrika. Kwa mfano toka ICC ianzishwe, miaka kumi ililiyopita imeshatangaza  watuhumiwa 32,ambao wote ni Waafrika, kwa maana hiyo viongozi wa Afrika ndio watu pekee wanaouwa watu kwa scale kubwa hapa duniani?

Kwa ufupi kesi ya Raisi Kenyatta haina miguu ya kusimama yenyewe, kesi ililetwa Mahakamani kutokana na mashahidi ambao wanasema walimsikia Raisi Kenyatta akiongea kuhusu kuwaajiri Mongiki (kikundi cha uterolisti cha Kenya) ili wawavamie kabila la Wakalenjin. Kati ya mashahidi hao shahidi mmoja tuu (shahidi numba 5) ndiye aliyetestifai kwamba kama alikuwepo wakati Raisi Kenyatta alipokuwa anawaajiri Mongiki.Na shahidi huyo ametolewa katika kesi hiyo kwa sababu za rushwa na uongo.

Kwa kifupi ICC  imechemsha kwenye uchaguzi wa Kenya,kwanza kwa kuleta mashitaka ya Raisi Kenyatta na makamu wake William Ruto katika kipindi ambacho siasa ilikuwa imechachamaa  nchini Kenya, katika kipindi cha uchaguzi mkuu.Kwani watu wote tunaelewa jambo lolote linalokuja wakati wa uchaguzi lazima liwe na siasa ndani yake.

Pili , Kwa  kawaida kabla kesi haijafunguliwa, Mwendesha mashitaka anapeleleza kesi kuona uzito wake na kukagua sehemu mauwaji yalipotokea (crime scene) kabla hajaipeleka kesi  mahakamani. Kwenye kesi ya Raisi Kenyatta ilikuwa ni kinyume. Luis Gabriel Moreno Ocampo, mwendesha mashitaka wa ICC aliifungua kesi ya Raisi Kenyatta na washitakiwa wengine kutokana na ripoti  zilizo wasilishwa kwake. ICC haukutuma Waendesha mashitaka wake nchini Kenya kuchunguza mauwaji ,kuongea na mashahidi, kuongea na waathirika wa pande zote kabla haijaifungua kesi, na hilo lilikuwa kosa  kubwa sana kwa upande wa ICC.

Lakini kwa kuwa Koti  ya Kimataifa ilishindwa kufauata hivi vipengele viwili,koti hiyo imejikuta ikiingizwa kwenye uchaguzi kama chombo cha kampeni na kupigwa kama mpira wa miguu na matokeo yake imepoteza heshima yake yote ndani ya Bara la Afrika.

Mwisho.