NGULI WA FILAMU TANZANIA-HEMEDI ALA SHAVU NONO!


Muigizaji wa filamu nchini Hemedy Suleiman aka PHD amekula shavu la nguvu la kupewa mkataba na kampuni moja ya usambazaji nchini kuigiza filamu saba kwa mwaka.

Akiongea na gazeti la Mwananchi, Hemedy alisema mkataba huo utamfanya yeye kufikiria zaidi filamu zake kuliko kucheza kwenye filamu za watu wengine.
Aliliambia gazeti hilo kuwa ubize huo wa mwaka pia ndo unamfanya kushindwa kuanza kutengeneza nguo za ndani za wanawake kama alivyosema mwaka huu kuwa anatarajia kuanza kubuni nguo zake za kike za ndani za wanawake.
“Watu kila siku wanajitokeza wanabuni tisheti, makoti na vitu vingine, mimi nilikaa chini nikafikiria kwanini mama zetu, dada zetu wanaenda kununua nguo za ndani za mtumba Mwenge na kwenye masoko mengine? Nikaona si kitu kizuri kwa kuwa hizo zimetoka nje ya nchi na zimeshavaliwa kwa hiyo mimi ndo nikaona nibuni nguo za ndani kwa ajili yao,”aliliambia gazeti hilo la kila siku.
Pia alidai kuwa ana mpango wa kurudi shule kumalizia ‘Degree’ yake ya Masoko ambayo alishaanza lakini alishindwa kuendelea kutokana na kazi.