MUIGIZAJI- LULU KUFANYA MAZUNGUMZO NA VYOMBO VYA HABARI !!


        
Baada ya kimya kingi kupita cha  muigizaji Elizabeth Michael a.k.a Lulu kupita  baada ya kutoka jela kwa dhamana kwenye kesi aliyokuwa nayo. Hatimaye blog hii  imepata habari za uhakika kutoka kwa mtu aliyehusika karibu zaidi na Lulu tangu akiwa anaanza kwenye uigizaji hadi alivyokuwa mahabusu kwenye kwa kesi yake na hadi kutoka. Sio mwingine bali ni Dr Cheni,
Na hii ni kauli yake
“Watu au media nyingi zinataka kufanya mahojiano na Lulu, hakuna anayejua nia ya mtu yoyote kwa sasa. Hataweza kwenda kilam media na kuzungumza na kila mwandishi, ukizingatia mazingira haliyotoka na umri wake anahitaji kupumzika sana, lakini ni kwamba tutafanya press conference hivi karibuni na mambo kadhaa tutayazungumza. Kwasababu mchakato wa kesi haujaisha kila kitu lazima kiennde kwa utaratibu. Siwezi kukwambia ni siku gani kwasababu inaitaji arrangement ilitufanye hiyo press conference. Kama tunavyoongea hapa nitakujulisha lini tunafanya baada ya muda mfupi na watanzania wasome kupitia hapa.” - Dr Cheni