BREAKING NEWS...MHESHIMIWA LEMA ARUDISHIWA UBUNGE WAKE!

lema


Hatimaye aliyekuwa mbunge wa Arusha Godbless Lema amekuwa tena mbunge wa Arusha baada ya kushinda katika rufaa ya kesi yake ya kupinga matokeo.
Rufaa hiyo imesomwa leo jijini Dar es Salaam.
Lema alivuliwa ubunge Aprili 5, 2012 katika hukumu iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibalira, kutokana na kesi iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM; Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
         ALAFU MNASEMA HATA MAHAKAMA NIZA CCM......HILI JE ???APANA CHEZEA MAHAKAMA!