MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Langa Mengisen Kileo, leo jioni amefariki katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar baada ya kuugua malaria na kisha kujitokeza homa ya uti wa mgongo.
Akizungumza na matandao wa GLOBAL PUBLISHER, baba mzazi wa Langa, Mzee Mengesen Kileo, amesema alimpeleka mwanaye Hospitali ya Kinondoni maarufu ‘Kwa Dokta Mvungi’ ambapo aligundulika kuwa na malaria na baadaye aligundulika kuwa na homa ya uti wa mgongo. Mzee Mengisen aliongeza kuwa, baada ya Dokta Mvungi kugundua kuwa Langa ana homa ya uti wa mgongo ambayo ni hatari, leo asubuhi aliamua kumkimbiza hospitali ya Muhimbili na kumfikishia chumba cha wagonjwa mahututi ‘ICU’. Baba huyo wa marehemu alizidi kuueleza mtandao huu kuwa, ilipofika mida ya saa kumi jioni, mwanaye aliaga dunia. Mipango ya mazishi inaendelea kupangwa nyumbani kwao marehemu Mtaa wa Chato, Mikochocheni jijini Dar.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU PEPONI !!