BONGO MOVIE TUTAFIKA KWELI???


   Kweli Bongo Movie Tutafika kweli??
Mwanadada Irene Uwoya amepost Picha hii kwenye Instagram yake akionyesha kuwa alikuwa Location akishoot Movie.Tatizo ni kwamba katika picha hiyo inamuonyesha jambazi aliyemvamia Irene nyumbani kwake lakini kabla ya kuvamia alivua Viatu.
   Je tangulini jambazi akaogopa kuchafua nyumba aliyoivamia,Director wa Movie hii ni nani?????

LUCCI KUDONDOSHA "SUMU" YAKE TAREHE 13 OCTOBER!


Ikiwa ni takribani mwezi mmoja umepita toka producer wa audio wa studio ya Transformax, Luciano Gadie Tsere maarufu kama Lucci aachie video ya duet yake na mrembo Jokate Mwegelo ‘Kaka/Dada’, producer huyo anategemea kuachia video mpya ya wimbo unaoitwa ‘SUMU’. Director Nisher ambaye jina lake linaendelea kukua kutokana na kazi anazoendelea kufanya ndiye aliyehusika kuandaa Video hiyo ya SUMU.Kama Flyer hiyo inavyoonyesha Siku moja tu imebaki.Tembelea hapa kesho kujionea mwenyewe hiyo SUMU.

FROM NIGERIA "P-SQUARE SASA KUTUA BONGO NOVEMBER 23!

002.JP

004.JP
    Mtangazaji wa East Afrika Radio, Hillary Daudi (Zembwela)akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza ujio wa wasanii wa muziki wa kizazi kipya Peter na Paul Okoye maarufu kama  P – Square  kutoka nchini Nigeria pamoja na mdhamini Mkuu,Tarehe 23 Mwezi ujao ndipo watawasili nchini. Wasanii hao wataambatana na wasanii wengine 13 kutoka nchini humo. Pamoja nae katika Picha ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasilino wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa ambo ndio wadhamini wa onesho hilo.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt jijini Dar, Hillary Daudi wa East Afrika Radio, Amesema onesho hilo litakuwa la kipekee. P- Square wataongozana na wasanii wengine 13 ambao watatoa burudani ya Live Band siku hiyo Pamoja na wasanii wengine kutoka Tanzania.Wote tunatambua namna kundi hili linavyofanya vizuri ndani na nje ya bara la Afrika, licha ya kutoa burudani kwa mashabiki, pia litatoa fursa kwa wasanii wa ndani kujifunza kutoka kwa wasanii hawa vijana ambao wamepata mafanikio makubwa kutokana na kazi yao ya muziki,” alisema na kuongeza “hii itakuwa ni fursa ya kipekee kwa wasanii wetu wa bongo kujifunza kwa kuangalia wenzao wanavyofanya kazi”. Tutaendelea kuwaletea Habari zaidi za tour hiyo.

SALOME AANGUSHA DINNER LA NGUVU KWA AJIRI YA OMMY DIMPOZ NYUMBANI KWAKE MARYLAND !

SALOME NA MGENI WAKE OMMY DIMPOZ KATIKA POZ
Baadhi ya Waalikwa akiwemo Promoter "DMK" katika Picha wakati wa chakula nyumbani kwa Salome Frederick Maryland.Salome alimwalika Dimpoz Pamoja na Baadhi ya Marafiki zake katika Chakula cha jioni kilicho andaliwa nyumbani kwake.Mbali na chakula Pia watu waliburudika na Vinywaji laini laini hadi majogoo.
SALOME KATIKA  POZ LA KUSIMAMA na MR POZ KWA POZ 
QUIZELA AKIWA KATIKA POZ NA OMMY DIMPOZ
Habari za Kuaminika nikuwa Dinpoz anapenda sana Watoto ebu angalia akiwafundisha mapoz
Dimpoz katika Picha ya Pamoja na Baadhi ya Wageni Waalikwa wa Dinner hiyo Nyumbani Kwa Salome
Dimpoz the Uncle katika Poz na Model wa Salome "Nyambona"

JUSTINE TIMBERLAKE AND ROBINTHICKE TO PERFORM FOR PHARELL WEDDING PARTY!

              
    Imethibitishwa kuwa Robin Thicke na Justine Timberlake ndio watakao tumbuiza kwenye sherehe za Harusi ya Producer Maarufu Pharel Williams.Sherehe hizo zitafanyika Miami ambapo zitakuwa nisherehe tu kwani Harusi ilifungwa kimya kimya mwezi August huko France.
   Pharell amemua Model na Designer maarufu Helen Lasichanah ambaye pia ni baby mama wake.Pharell ni producer maarufu aliyefanya kazi na wanamuziki mbalimbali kama Jay Z,Kanye,Beyonce,Madona na wengine wengi hivyo tutegemee guest list ya Mastaa karibu wote.

KELLY ROWLAND ATUMBUIZA KWA PESA NYINGI AFRICA YA KUSINI.


Kelly Rowland atumbuiza kwenye private party ya bilionea mkubwa wa Africa ya Kusini Douw Styn

JUMBA LA KIFAHARI LA BILIONEA HUYO WA SOUTH AFRICA
Kelly Rowland aliwasili Nchini humo tarehe 25 sept kwa ajili ya Party ya siku mbili iliyokuwa imepangwa kufanyika kabla Mandela hajawa mgonjwa na ndiye aliyekuwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwani ni rafiki mkubwa wa bilionea huyo.

KIJIWE CHA UGHAIBUNI NA VIJIMAMBO

BIASHARA MATANGAZO !

Yaani Sio Mabango tu


Na Joseph Msami wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Matifa

Mfanyabiashara huyu mwenye asili ya Uhispania ambaye jina lake halikufahamika mara moja alinaswa katikati ya mji wa New York akiwa amevaa mabango yanayotangaza mavazi ya wanaume (suti) na kusambaza vipeperushi vinavyoelekeza wapi bidhaa hizo zinapatikana pamoja na mawasiliano.
Asili ya wakazi wa mji huu, kutingwa na shughuli na kutembea mwendo kasi muda mwingi kunawalazimu wafanyabiashara kubadili mbinu za kufikisha ujumbe wao ambapo badala ya kuongea na watu,wengi hutoa kadi za biashara zenye mawasiliano (business cards) au kuweka mabango yenye ujumbe husika.

FAY DESTINY APATA USHINDI KWENYE TAMASHA LA KIMATAIFA LA MUZIKI WA INJILI MAREKANI.

                 1371356_10200791039954422_687147133_n
  1383470_10200554420324634_318863772_n
Fay Jukwaani. Mwanamuziki wa Injili anayeibukia miongoni mwa Watanzania hapa Marekani ni Bibie Fay Makame Haji a.k.a Fay Destiny mwanadada huyu mwenye asili ya visiwani Zanzibar, ambaye pia alibadili dini kutoka Uislam na kingia Ukristo alishiriki hivi karibuni kwenye mashindano ya uimbaji wa nyimbo za Injili wa kimataifa kwa nchi za Afrika katika jiji la Maryland na kufanikiwa kunyakua nafasi ya tatu ambapo alikumbana na washindani kutoka nchi nyingine mbali mbali za Afrika zikiwamo Nigeria, Liberia, Ethiopia,Sierra Leone n.k. Fay ameshatamba sana na kibao chake kiitwacho Inuka na nyimbo mbali mbali na baada ya kupepersha vyema bendera ya Tanzania kwenye michuano hiyo pia Fay alipata nafasi ya kufanya mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika (VOA) hapa Washington Dc na kusikiliza mahojiano hayo bofya hapa. [audio http://sundayshomari.files.wordpress.com/2013/10/mahojiano-na-fay-destiny.mp3] Wakati huo huo Fay Destiny anatarajia kuzindua albam yake ya kwanza Jumamosi huko katika ukumbi wa Hmpton Inn Hotel siku ya Jumamosi Oktoba 5,2013. ambapo atasindikizwa na wanamuziki kadhaa wa Injili wakiwamo kundi maarufu la JJ Sisters, Pastor Baraza na wengineo.Msikilize hapa akitoa habari hiyo kwa ukamilifu.